AFISA MASOKO MWANDAMIZI WA POSTA MAKAO MAKUU KALOLINE KANUTI AKIWA NA WATOTO WA KITUO CHA MTAKATIFU JUSTINE BAADA YA KUTOA MSAADA |
MENEJA WA PSTA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIJANA WA KITUO CHA MTAKATIFU JUSTINE NA WAFANYAKAZI WA POSTA |
MWENDO WA MCHELE MBUZI
WATOTO WENYE UHITAJI TUWAKUMBUKE
LECHA YA ULEMAVU WATOTO HAWA WASIO SIKIA WALISHIRIKIA MASHINDANO YA KITAIFA YA RIADHA JIJINI DAR ES SALAAM
PAMOJA TUWALEE
LICHA ULEMAVU ANAFANYA VIZURI SANA DARASANI
Jamii imetakiwa kujenga utamaduni wa kusaidia watu walio
kwenye uhitaji ili waweze kuondokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili na
kuifanya jamii husika kuishi kama binadamu wengine bila kujiona wanyonge na
wapweke waliosahalika.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Shirika la Posta mkoani
Mara Bakari Kombo Bakari alipokuwa akikabidhi misaada mbalimbali ya kijamii
ikiwemo mchele,mbuzi mnyama,mafuta ya kupikia pamoja na sabuni katika kituo cha
kulea watoto wenye ulemavu na yatima cha Mtakatifu Justine kilichopo Manispaa
ya Musoma ikiwa ni maadhimisho ya siku ya posta duniani.
Amesema kwa namna walivyokitembelea kituo hicho na kukutana
na changamoto mbalimbali zinazowakabili jamii inapaswa kuona umuhimu wa kuwasaidia ili
waweze kuondokana na adha zinazowakabili katika kituo hicho.
Meneja huyo wa posta amesema watoto wenye ulemavu ukiwemo wa
akili,viziwi na viungo walipo kwenye kituo hicho wanahitaji misaada ikiwemo
chakula na mahitaji mengine kwa mujibu wa wasimamizi wa kituo hicho hivyo jamii
inapaswa kuliangalia na kuona umuhimu wa kuwasaidia.
Amesema Shirika la posta ikiwa ni moja ya jukumu lao kutoa
misaada katika jamii yenye uhitaji lakini kazi hiyo haiwezi kufanya na upande
mmoja bali kila mmoja anawajibika kuguswa na changamoto walizonazo watoto hao
na kuweza kuwasaidia
Kwa upande wake Muangalizi mkuu wa kituo hicho sister
Magreth John amelishukuru Shirika la posta kwa msaada waliopa baada ya
kuwatembelea na kuomba watu wengine kuguswa na mazingira waliyokuwa nayo watoto
wenye ulemavu na yatima na kuwapa msaada wa kibinadamu.
Amesema kituo hicho chenye jumla ya watoto 130 wenye ulemavu
mbalimbali wanakabiliwa na uhaba wa chakula kwenye kituo nakusema mtu yoyote
anaweza kuwatembelea kwenye kituo hicho kilichop[o makoko na kuwapa msaada.
No comments:
Post a Comment