TAARIFA
KWA UMMA
Katika Gazeti la Mawio Toleo Namba 0062 la
tarehe 26.9.2013 – 02.10.2013 na toleo Namba 0063 la tarehe 03.10.2013
zimechapishwa habari zenye vichwa vya habari “Mtandao wa Ujangili Huu Hapa”
na “Wabunge
CCM watajwa ujangili”.
Katika habari zote hizo zimelihusisa
shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama chanzo cha habari hizo.
Shirika
la Hifadhi za Taifa linapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusiana na taarifa
hizi:
(i)
Shirika
la Hifadhi za Taifa halijawahi kudhamini ripoti iliyotajwa katika habari hizo
kuhusiana na utafiti makini wa ujangili.
(ii)
Shirika husimamia shughuli za uhifadhi katika
maeneo ya Hifadhi
za Taifa pekee kiutendaji, ambapo
baadhi ya maeneo yaliyotajwa
Katika habari hizo kama Selous na
Liwale kiutendaji hayapo ndani
ya Shirika la Hifadhi za Taifa.
(iii)
Kama
Shirika la Umma, hufuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kushirikisha
vyombo mbalimbali vya dola katika kushughulikia uhalifu wa aina mbalimbali
ikiwemo ujangili.
Ni
kwa mantiki hii basi, shirika linapenda kuweka bayana kuwa halihusiki na
taarifa hizo, na hata pale zinapopokelewa zina utaratibu wake wa kufanyia kazi.
Tunachukua nafasi hii kuviomba vyombo vya
habari kushiriki katika juhudi za kupambana na ujangili kwa kuwa waangalifu
katika kuandika habari za kutuhumiana kabla ya kuwa na ushahidi kamili ambao ni
haki ya kimsingi ya kisheria inayopaswa kuheshimiwa.
Imetolewa na Idara
ya Uhusiano
HIFADHI
ZA TAIFA TANZANIA
07/10/2013
No comments:
Post a Comment