Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Serengeti Bw
John Ng’oina akiongea na blog hii ametoa Pongezi hizo kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati akiileza Channel ten hali ya ujenzi wa
hospital hiyo.
Amesema hospital hiyo ambayo itakuwa ya ghorofa sita
na vifaa vya kisasa itakuwa na Msaada mkubwa katika wilaya hiyo ambapo kwasasa
wapo kwenye mchakato wa kutafuta fedha ili kukamilisha ujenzi huo.
Mbali na Mradi wa ujenzi wa Hospital hiyo lakini pia
ujenzi wa kiwanja cha Ndege na Chuo kikuu kitivo cha Mali asili na utalii
imeelezwa itasaidia kuinua hamasa ya elimu katika halamashauri hiyokama
wanavyoeleza baadhi ya Madiwani wa halmashauri hiyo.
Ujenzi wa hospital hiyo ya wilaya unafanyika umbali wa
kilomita 3 kutoka Makao Makuu ya wilaya hiyo katika eneo la Kibeyo ambapo
umeanza Mwaka 2008/ 2009 huku ikikadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilion
13 huku tayari awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la OPD umefanyika ikiwa
pamoja na kulipa fidia kwa Wananchi waliokuwa karibu na eneo la Mradi
No comments:
Post a Comment