Wadau wa masuala ya sheria nchini
Tanzania wametakiwa kuweka utaratibu wa kisheria ambao utasaidia kuzuia
vitendo vya utoaji mimba tofauti na taratibu zilizopo hivi sasa ambazo
zinaonekana kushindwa.
Mwanachama
wa Chama cha Wanasheria wanawake nchini Tanzania TAWLA Bi. Anna Marie
amesema hayo wakati akitoa mada kwa wanahabari juu ya tatizo la utoaji
mimba ambalo hivi sasa linaonekana kushamiri nchini.
Bi. Marie amesema licha ya kuwepo kwa
sheria ya kuzuia utoaji mimba, sheria hiyo imekuwa kama haifanyi kazi
kutokana na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na vitendo vyenyewe kufanyika
katika mazingira ya siri.
No comments:
Post a Comment