Taasisi ya kuhamasisha maendeleo na
mawasiliano katika jamii yenye makao yake mjini Musoma mkoani Mara ya JAMII INFORMATION NETWORK inatarajia
kufanya Kongamano kubwa litakalo wahusisha Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka Shule 10 za
Sekondari za Manispaa ya Musoma Mwezi August Mwaka huu, ikiwa ni njia ya kuhamasisha Maendeleo na kuimarishaji wa Mawasiliano
ndani ya Jamii.
Katika
Kongamano hilo mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu waliobobea katika Masuala
uhamasishaji wa Vijana Kupambana dhidi ya Ukimwi,ujasiriamali,dhana ya
kujiajiri,Changamoto katika Elimu kwa Vijana
pamoja na Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni njia ya kujenga Msingi bora wa
Makuzi kwa Vijana wetu.
Mbali
na hivyo vijana hao pia wataelezwa jinsi ya kuwa Wazalendo katika nchi
yao,kupambana na rushwa,Umaskini lakini pia wakipata elimu sahihi ya faida za
uwekezaji kwa Tanzania,Sababu za Mimba za Mapema kwa watoto wa kike na jinsi ya
kujenga Mahusiano na Mawasiliano yaliyo sahihi.
Pamoja
na Mtandao huu kuwa na nia njema katika kuwasaidia Vijana lakini bado
kumekuwepo na Changamoto mbalimbali katika kufanikisha Kongamano hilo hasa
katika Suala la kifedha,hivyo basi Taasisi ya JAMII INFORMATION NETWORK kwa nia njema inakuomba wewe
Mtanzania,Mpenda Maendeleo,unaekaa ndani au nje ya nchi,Mashirika kusaidia Taasisi
hii katika kufanikisha Kongamano hilo ili vijana wetu wakue katika Makuzi mema
na kujenga Tanzania ya kesho
iliyostaarabika.
Blog Master
Jamii.information@yahoo.com
No comments:
Post a Comment