Friday, May 10, 2013

ASKARI ALIYEUA TARIME CHINI YA ULINZI

Mwanafunzi mmoja wa darasa la kwanza katika shule ya msingi rebu wilayani tarime mkoani mara deus jacob,ameuawa kinyama baada ya kupigwa risasi kichwani na askari polisi wa  wilayani tarime  wakati  wakiwa katika harakati za kumkamata  mtuhumiwa wa kosa la kushambulia na kujeruhi.
 
 
kamanda wa polisi kanda maalum ya tarime rorya,kamishina msaidizi  justus kamugisha,amesema mwanafunzi huyo mkazi wa songambele wilayani tarime amepigwa risasi hiyo ambayo imesababisha kupoteza maisha na askari polisi mwenye namba d 4662 koplo methew  wakati akipita barabarani.
 
kamanda kamugisha amesema kuwa risasi hiyo ambayo imemuawa mwanafunzi huyo ni miongoni mwa risasi tano ambazo zilifyatuka wakati wa porukushani  ikihusisha mtuhumiwa  huyo marwa chacha na  askari polisi katika jaribio la kupora bunduki.
 
kwa mujibu wa kamanda kamugisha  askari polisi huyo anashikiriwa kwa mahojiano wakati wakimtafuta mtuhumiwa marw chacha  ambaye alikimbia baada ya tukio hilo kutokea  ambapo polisi walifanikiwsa kukamata misokoto ya bangi 45 na kilo 3 na roba za bangi kavu ambayo inadaiwa ni mali ya mtuhumiwa huyo.
 
kwa upande wake mzazi wa mwanafunzi huyo mzee jacob mwita sasi,amelaani kitendo cha polisi huyo kumua mtoto wake kwa risasi bila kosa hivyo kutaka vyombo vya sheria kuchukua harua ili kuhakikisha haki inatendeka.

No comments:

Post a Comment