HALMASHAURI YATAKIWA KUDHIBITI MAPATO.
Dinna Maningo,Rorya.
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara
wameitaka Halmashauri hiyo kutafuta wataalamu kutafiti namna ya kupata vyanzo
vya mapato ili iweze kukua kimapato badala ya kusubiri ruzuku kutoka
Serikalini.
Wakiongea kwenye kikao cha baraza la madiwani madiwani hao
walisema kuwa Wilaya ya Rorya ina vyanzo vingi vya mapato lakini pato linalopatikana
haliendani na vyanzo vilivyopo jambo linalosababisha kutoongezeka kwa pato la
ndani la halmashauri na badala yake kungoja pesa za ruzuku ya Serikali
kutekeleza mahitaji ambapo ruzuku hiyo haitoshelezi.
Diwani wa kata ya Kisumwa Piter Malaki (NCCR) amesema kuwa Pato
la Halmashauri halikuwi licha yakuwa kuna vyanzo vingi na hivyo kuoba watafutwe wataalamu watakaopitia na kufanya utafiti
wa kujua na kupata vyanzo vya ndani vya
mapato badala ya kungoja ruzuku kutoka Serikalini
ambayo haifiki kwa wakati.
Diwani wa Tarafa ya Nyancha Pendo Odelle( CCM) amesema usimamizi
mbovu wa mapato ya ndani ndiyo uchangia
kutoongezeka kwa pato kwani halmashauri imeshindwa kufatilia na
kujua namna ya ukusanyaji mapato
unavyofanyika hususani kwa mawakala wanaokusanya ushuru kwa madai kuwa kuna
mawakala wamekuwa wandanganyifu ambapo ukusanya pesa nyingi huku halmashauri
ikipata pato kidogo.
Diwani wa kata ya ya Kitembe Thomas Patrick(CHADEMA) amesema
bila kusimamia mapato ya ndani halmashauri
haiwezi kusonga kwa madai kuwa
soko la Obwele lililoko Shirati limekuwa likipoteza mapato mengi kutoka na na
uzembe wa ukusanyaji mapato kutokana na wakusanyajiushuru kukaa kando na
kungoja wafanya biashara wawapelekee pesa ya ushuru ambapo wengine uondoka bila
kulipaushuru.
Diwani wa kata ya Ikoma Laulent Adriano(CCM) amesema kuwa
tatizo ni halmashauri kutotoa viwango halisi vya ushuru wa bidhaa zinazotozwa
kwakuwa kuna watendaji wa kata na vijiji wamekuwa wakitoza wananchi viwango vikubwa isivyo halali na kuwafanya kukwepa ushuru.
Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Rorya Andreas Madundo amesema
kuwa inawezekana kufanya utafiti wa kina wa vyanzo vya mapato lakini kufikia
lengo itakuwa ni juhudi za ziada kwa
madai kuwa tangu kustishwa kwa ruzuku za fidia kumechsangia halmashauri
kutofikia malengo yake kwani makusanyo yanayopatikana ni kidogo ukilinganisha
na vyanzo vichache vya mapato vilivyoko
ndani ya halmashauri hiyo.
Halamshauri ya Rorya kwa kipindi cha Julai 2011- juni 2012
vyanzo vya halmashauri makisio 2011/2012
ni 1,491,977,00.00,makusanyo julai 2011-mei 2012 ni 573, 104,098.00,makusanyo juni 2012 ni
22,105,637.00 ambapo jumla ya mapato kutoka julai 2011 –juni 2012 ni
595,209,735.00 sawa na asilimia 40%.
Wakati huo huo,
MKUU wa Wilaya ya Rorya Elias Goroi ameahidi kusimamia
mapato ya halmashauri ya wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha za miradi zinazotolewa inatekelezwa kwa
wakati.
DC Goroi alisema kuwa mapato ya halmashauri yanapaswa
kuongezeka na siyo kila mwaka mkaguzi anakuta mapungufu na kuwa kwa wale
watakao bainika katika matumizi mabaya
ya fedha watachukuliwa hatua za
kisheria
Aliongeza kuwa Halmashauri inapaswa kuhakikisha pesa zinazotolewa zinatumika
vizuri na kwamba nidahamu itumike katika ukusanyanji wa mapato wilayani Rorya
kwakuwa pesa hizo ni za wananchi.
No comments:
Post a Comment