WAUMINI WA DINI YA KIISLAM WATAKIWA KUZINGATIA KUTOA ZAKA
Na Shomari Binda
Musoma,
Waumini wa Dini ya Kiislam wametakiwa kuzingatia suala la utoaji wa
zakar tul fitri kipindi hiki ambacho mwezi mtukufu wa Ramadhani
unaelekea ukingoni ili kuifanya funga ya swaumu ipate mapokeo mazuri kwa
Mwenyezi Mungu kwa pale palipoonekana palikuwa na mapungufu katika
funga.
Wito huo umetolewa leo na Ustadhi Suleimani Musa Magoti
baada ya kumalizika kwa swala ya Ishaa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa
Mjini Musoma alipokuwa akiwakumbusha waumini wa Dini ya Kiislamu
kuhusiana na suala hilo.
Amesema suala la kutoa Zaka lina
umuhimu mkubwa kwa Muumini na kila mmoja mwenye uwezo wa kutoa zaka
anapaswa kufanya hivyo bila kupuuzia kutokana na mafundisho
yanayopatikana katika jambo zima la kutoa zaka.
Ameeleza kuwa
muumini anapokuwa katika funga kutokana na ubinadamu anaweza kujikuta
amekosema jambo furani iwe ni kutokana na urimi ama matendo hivyo zaka
inasafisha makosa kama hayo na kufanya funga ya muumini ipate kupokelewa
na Mwenyezi Mungu.
Ustadhi Suleimani amedai Muislam asikubali
Ramadhani ikamalizika bila kujilidhisha katika funga yake kwa kutoa zaka
kwa mwenye uwezo wa kufanya hivyo kutokana na umuhimu wake.
Aidha amesisitiza kuzingatia jamii inayopaswa kupewa zaka kwa mujibu wa
mafundisho na kuepuka kuwapa zaka watu kama walevi,wasio fanya ibada na
funga na wale wenye uwezo bali wapewe masikini na mafukara na wale walio
kwenye matatizo kama wafungwa na wazee wasio jiweza.
Zakar Tul
Fitri utolewa siku chache kabla ya kumalizika mfungo wa Mwezi Mtukufu
wa Ramadhani na muda mchache kabla ya kuswaliwa kwa swala ya Eid el
Fitri.
Ramadhani Kareem.
Wito huo umetolewa leo na Ustadhi Suleimani Musa Magoti baada ya kumalizika kwa swala ya Ishaa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mjini Musoma alipokuwa akiwakumbusha waumini wa Dini ya Kiislamu kuhusiana na suala hilo.
Amesema suala la kutoa Zaka lina umuhimu mkubwa kwa Muumini na kila mmoja mwenye uwezo wa kutoa zaka anapaswa kufanya hivyo bila kupuuzia kutokana na mafundisho yanayopatikana katika jambo zima la kutoa zaka.
Ameeleza kuwa muumini anapokuwa katika funga kutokana na ubinadamu anaweza kujikuta amekosema jambo furani iwe ni kutokana na urimi ama matendo hivyo zaka inasafisha makosa kama hayo na kufanya funga ya muumini ipate kupokelewa na Mwenyezi Mungu.
Ustadhi Suleimani amedai Muislam asikubali Ramadhani ikamalizika bila kujilidhisha katika funga yake kwa kutoa zaka kwa mwenye uwezo wa kufanya hivyo kutokana na umuhimu wake.
Aidha amesisitiza kuzingatia jamii inayopaswa kupewa zaka kwa mujibu wa mafundisho na kuepuka kuwapa zaka watu kama walevi,wasio fanya ibada na funga na wale wenye uwezo bali wapewe masikini na mafukara na wale walio kwenye matatizo kama wafungwa na wazee wasio jiweza.
Zakar Tul Fitri utolewa siku chache kabla ya kumalizika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na muda mchache kabla ya kuswaliwa kwa swala ya Eid el Fitri.
Ramadhani Kareem.
No comments:
Post a Comment