SERIKALI :VIWANGO VIPYA VYA SUMATRA
NDIVYO VITAKAVYOTUMIKA.
Dinna
Maningo,Tarime
SERIKALI
imesema kuwa viwango vipya vya nauli vilivyotolewa na Mamlaka ya
usafirishaji majini na Nchi kavu SUMATRA
ndivyo vitakavyotumika katika magari yanayofanya usafirishaji wa Abiria ndani ya Wilaya ya
Tarime hadi Musoma nakwamba mgomo wa siku mbili uliofanywa na wamiliki wa
magari si halali bali ulikuwa ni
kuwatesa wananchi.
Hayo yamebainika
kwenye kikao cha utatuzi wa mgomo wa wamiliki wa magari Tarime wa magari yao kutofanya usafiri Wilayani
Tarime hadi Musoma Kilichofanyika ndani ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime kilichowakutanisha
wawakilishi wasafirishaji,baadhi ya viongozi wa Polisi,Ofisa Mfawidhi wa
SUMATRA Mkoa wa Mara Maico Rojasi na Mkuu wa Wilya ya Tarime John Henjewele.
Mkuu wa
Wilaya ya Tarime John Henjewele alisema kuwa
kikao kimebaini kuwa wasafirishaji walikuwa na mgomo wa kutotoa
huduma ya usafiri na kwamba wamiliki
walifanya mgomo kabla ya kutoa malalamiko yao ofisi ya Mkuu wa wilaya na kwamba
mgomo ni batiri kwakuwa hakuna taasisi yoyote inayotoa magari ya
uisafirishaji iliyosajiriwa kisheria Richa ya wao kufanya mgomo hivyo viwango vipya
ndivyo vitakavyotumika
“Tumefanya
kikao na wawakilishi wa usafirishaji wakiwamo baadhi ya viongozi wa Serikali
kikao kimebaini kweli kulikuwa na mgomo wa siku
2 wamiliki wenyewe wamekili makosa yao, pia wakati wa mgomo wao
hawakuijulisha Serikali bali wamekuwa wakiwasiliana na Sumatra Pekee na mgomo
huo ni wa makundi na wala taasisi zao za magari ya usafirishaji hazina usajiri
kwahiyo viwango vipya vya serikali viendelee kutumika watakaokiuka
watawajibishwa kisheria”alisema Henjewele.
Ofisa Mfawidhi
wa mamlaka ya usafirishaji majini na nchi kavu SUMATRA Mkoa wa Mara Maico
Rojasi alisema kuwa kwa yale magari madogo maarufu kama mchomoko yanatakiwa
kutotoa huduma ya usafilishaji na kwamba yanatakiwa kufanya kazi kwa kukodiwa
kama vile Tax kwakuwa ndiyo vyanzo vikubwa vya nauli kupanda na kwamba uamuzi
huo hauwazuii wao kuomba kuongeza kupandishwa kwa viwango iwapo wanasababu za
msingi.
Kwa upande
wa wawakilishi wasafirishaji wakiwakilishwa na katibu wao Stephano Keraryo wamekili
kuwa na mapungufu likiwamo la kufanya mgomo bila kuifahamisha Serikali hususani
Mkuu wa Wilaya ya Tarime John Henjewele na chama chao cha wasafirishaji
kutokuwa na usajiri ambapo wamekubali kuendelea na huduma ya usafirishaji kwa
viwango vipywa wakati huo wakifanya taratibu zingine za kuomba kupandishwa kwa
nauli
No comments:
Post a Comment