Wiki hii aliyekuwa naibu katibu mkuu wa
umoja wa mataifa Dr.Asha Rose Migiro amerejea nchini baada ya
kuutumikia kwa miaka mitano.
Hata hivyo shirika la habari la Vox Media limebaini sababu za kwanini
Dr. Migiro hakuongezewa muda wa kufanya kazi kwenye umoja huo.
Limesema vyanzo vya ndani ya UN vimesnitch kuwa utendaji dhaifu na
kushindwa kufit kwenye chombo hicho kigumu ni baadhi ya sababu ya
kushindwa kuongezewa mkataba wa kufanya kazi humo.
“Nafasi ya Unaibu katibu mkuu ni ngumu mno; inahitaji mtu mzoefu
kuongoza vema Secretariat. Changamoto yake kubwa ilikuwa ni kuelewa
siasa katika chombo hicho cha kimataifa na kuunda muungano,” chanzo
kimoja kiliiambia Vox Media.
Inadaiwa kuwa Dr. Migiro alizungumza na kundi la waafrika lenye asilimia
28 ya wajumbe wa umoja wa mataifa ili achaguliwe tena lakini
walimtosa.
“Hakuwa maarufu miongoni wa wanadiplomasia. Hakuna aliyemsikiliza.
Unaweza kukumbuka pia kuwa uteuzi wake ulikosolewa sana,” kilisema
chanzo hicho.
Katika hatua nyingine Dr. Migiro alisema hana mpango wa kuwania urais wa
Tanzania na huenda akarejea kwenye kazi yake ya zamani ya uhadhiri wa
chuo kikuu.
Chanzo: Bongo 5

No comments:
Post a Comment