Tuesday, July 3, 2012

WARSHA YA PSI KATIKA UTAMBULISHO WA PROGRAM YA FAMILIA MKOANI MARA

Mmoja ya watumishi wa PSI mkoani Mwanza Ndg Rajabu Chuma
 Mkuu wa wilaya ya Musoma Ndg Jackson Msome akifungua Warsha ya PSI inayohusiana na Masuala ya Familia katika ukumbi wa Anglikana mjini Musoma
  Wadau wa mambo ya uzazi wa Mpango katika Warsha ya PSI mjini Musoma
                   Wadau wa uzazi wa Mpango
              Meza mkuu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Ushirikiano wa PSI ndg John Wanyanja,Mkuu wa wilaya ya Musoma na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara
  Wadau wa Uzazi wa Mpango wakifuatilia hiyo warsha kwa umakini mkubwa
 Viongozi wa Vyama vya siasa mkoani Mara wakiwa katika Warsha hiyo mjini Musoma

          George Marato wa ITV mkoani Mara
  Waandishi wa habari wakibadilishana mawazo na mkuu wa Wilaya ya Musoma Ndg Jackson Msome
  Mganga mkuu wa Mkoa wa Mara akitoa takwimu mbalimbali kuhusiana na sekta ya Afya mkoani Mara



 Sekta ya Afya mkoani Mara imekuwa na changamoto kubwa huku wadau mbalimbali wakijitokeza kusaidiana na Serikali katika kutatua changamoto hizo,katika Warsha iliyoandaliwa na PSI Tanzania ambayo inafanyika mkoani Mara wadau mbalimbali wameeleza changamoto hizo na njia ya kupambana nazo.

Mgeni rasmi katika Warsha hiyo mkuu wa Mkoa wa Mara Mh John Tuppa aliyewakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Musoma amesema mpango huu mpya wa PSI katika program ya Familia utakuwa chachu muhimu katika kuinua kiwango cha mpango wa uzazi mkoani Mara,amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanyika na taasisi ya Takwimu nchini (National Bureau of Statics) mnamo mwaka 2010 mkoa wa Mara ni wa Mwisho Tanzania bara ukiwa na kiwango cha asilimia 9.6 cha matumizi ya njia za kisasa za Mpango wa uzazi.


Katika tafiti hizo zilionyesha kuwa Mkoa wa Kilimanjaro ndio mkoa unaoongoza ukiwa na kiwango cha asilimi 50.3 cha matumizi ya  njia za kisasa za mpango wa uzazi


Kwa upande wake Mganga mkuu wa mkoa wa Mara Dr Samson Winani amesema kuwa changamoto hizo zinatokana na mkoa kutokuwa na Hospital ya Rufaa kitu kinachochangia huduma ya afya mkoani Mara kudhorota.

Amesema kwa sasa bado Serikali na wadau mbalimbali wanaendele ikiwa ni njia ya kutatua changamoto hizo mkoani Mara, kuhusu suala la Ukimwi mkoani Mara Dr Winani amesema kuwa kumekuwepo na Ongezeko la kasi kwa ugonjwa wa Ukimwi mkoani Mara ambapo kwa mwaka 2003 ongezeko lilikuwa la asilimia 3.3 huku mwaka 2008 ongezeko hilo lilifikia asilimia 7.7 huku wilaya ya Rorya mkoani Mara ikiwa ya pili kitaifa kwa ongezeko la kasi hiyo ambapo asilimi 13 ya wakazi wa huko wanaishi na virusi vya Ukimwi.

Aidha amesema changamoto nyingine ni vifo vya akina mama wajawazito wanaoshindwa kupata huduma mapema na kupelekea kupoteza Maisha huku akisema kwasasa mkoa wa Mara una vituo 11 vya huduma ya Afya huku kila wilaya ikiwa na vituo viwili.Ameongeza kuwa wataalam watapelekwa kila wilaya ambapo kwasasa kila wilaya imegawiwa pikipiki nne katika kusaidia wagonjwa.

Kuhusu Mgomo wa madaktari Dr Winani amesema kuwa Mazungumzo yalifanyika na madaktari wa Hospital yake ambapo alisema kuwa kutokana na uelewa wa Madaktari hao hawakuona umuhimu wa kugoma huku Serikali ikiendelea  kutatua matatizo mbalimbali.


Naye Mkurugenzi ushirikiano wa PSI Tanzania Ndg John Wanyanja amesema mafunzo yatolewayo na PSI kwa wadau yatasaidia wadau hao kupata elimu ya mbalimbali ikiwemo uzazi wa Mpnago  huku akisema kuwa kuna kiwango cha chini cha matumizi ya uzazi wa mpango ambapo takwimu kwa mwaka 2010 inaonyesha ni asilimi 9.6 pekee

No comments:

Post a Comment