LISTI ya FIFA UBORA DUNIANI: Hispania juu palepale huku Tanzania yapanda nafasi 12 ipo 127!
Tanzania
imependa kwa nafasi 12 kwenye orodha ya viwango vya ubora ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Julai 4 mwaka huu) na
shirikisho hilo.
Kwa viwango
vya Juni mwaka huu, Tanzania (Taifa Stars) ambayo timu yake inadhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 139 hivi sasa imefika nafasi ya 127
ikiwa na pointi 253 kulinganisha na 214 za Juni mwaka huu
Kikosi cha Taifa Stars
Ivory Coast
inayoshika nafasi ya 16 duniani bado inaongoza kwa upande wa Afrika ikiwa na
pointi 939. Timu hiyo ilikuwa katika nafasi hiyo hiyo kwa viwango vilivyotolewa
Juni 6 mwaka huu. Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia ndiyo
wanaoendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 1,691.
Hispania ,
ambao ndio Mabingwa wa Ulaya na Dunia, wameendelea kushika Nambari Wani kwenye
Listi ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani iliyotolewa leo huku Tanzania ikipanda
nafasi 12 na kushikilia Nambari 127.
Italia,
ambao walifungwa na Hispania kwenye Fainali ya EURO 2012 Jumapili iliyopita,
wamepanda nafasi 6 na kurudi tena kwenye 10 bora na sasa wako nafasi ya 6 huku
Portugal/Ureno wakipanda nafasi 5 na kukamata nafasi ya 5 ili hali Uingereza wamepanda nafasi mbili na kushika nafasi ya 4.
Listi
nyingine itatolewa Agosti 8.
20 BORA:
1 Hispania
2 Ujerumani
3 Uruguay
4 Uingereza
5 Portugal
6 Italia
7 Argentina
8 Uholanzi
9 Croatia
10 Denmark
11 Brazil
12 Greece
13 Russia
14 Ufaransa
15 Chile
16 Côte
d'Ivoire
17 Sweden
18 Czech
Republic
19 Mexico
20 Japan
No comments:
Post a Comment