TAARIFA RASMI KWA WANANCHI NA WAFANYAKAZI WOTE WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi ya tarehe 23 Juni 2012.
Baada
ya tathmini hiyo, Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo:(i)
Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;(ii)
Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama
Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria
ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.(iii)
Madaktari waliopo likizo warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia
likizo na nauli zao umeandaliwa. (iv) Uongozi wa
Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea
kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu
wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;(v) Uongozi wa
Hospitali ufute mara moja ‘rotations’ za Madaktari waliopo kwenye
mafunzo kwa vitendo (interns); na(vi) Uongozi wa
Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo
kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo
Aidha,
Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao
wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla. Vilevile,
Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na
subira na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na
maadili ya taaluma zao.
_________________
Dkt. Gabriel Upunda
KAIMU MWENYEKITI BODI YA WADHAMINI
No comments:
Post a Comment