Monday, July 2, 2012

                  POLISI TARIME WADIWA KUWAGEUZA WANANCHI MRADI.

Dinna Maningo,Tarime

MWENYEKITI wa Vijana Taifa kupitia Chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema (BAVICHA) John Heche Amewaonya Polisi wa Kanda maalumu ya Taime/Rorya wanaotumia vazi la uporisi na kisha kuwakamata wananchi ovyo hata wasio kuwa na hatia kwa kisingizio cha uvamizi wa Mgodi wa dhahabu Noth Mara na kwamba kitendo  hicho ni kuwafanya wanachi waishi bila amani.

Akiongea na waandishi wa habari Heche alisema kuwa tangu kuanza kwa oparesheni Tarime polisi wamekuwa wakiwakamata watu ovyo hususani wakazi wa Nyamongo ambao ukamatwa kwa visingizio vya uvamizi wa mgodi wa North Mara na kisha kupelekwa mahakamani ambapo utozwa dhamana ya sh.laki 3 kwa kila mtuhumiwa.
 
Alisema kuwa mbali na wanachi kukamatwa maeneo ya mgodi pia hata kwa wananchi ambao wamekuwa wakikamatwa kwa makosa mbalimbali tofauti ya uvamizi wa mgodi nao wamekuwa hawashitakiwi kwa kosa walilokamatiwa badala yake ubandikiziwa kesi ya uvamizi wa mgodi na mauwaji.
 
"Polisi Tarime wamewageuza wananchi vipato wanawakamata wanawabandikizia vesi vya uongo kisa tu wawapatie pesa mtu anakamatwa anapelekwa kituo cha polisi anatozwa hela zaidi ya shi laki 2 ili aachiwe kwa wale wa Nyamongo akikataa anapelekwa kituo cha polisi Wilaya ya kipolisi Nyamwaga nako anoombwa hela akikataa anapelekwa kituo cha polisi kikuu Bomani  nako anaombwa sh. laki mbili ili aachiwe huru akikataa  mtuhumiwa anaundiwa kesi na kupelekwa mahakamani ambapo kwa sasa wanaokamatwa ufikishwa mahakama ya Mwanzo mjini Tarime na kutozwa dhamana ya sh laki 3 kwa kila mtuhumiwa anayetuka Nyamongo"alisema Heche.
 
"Polisi wa Tarime wananufaika kupitia wananchi wanawakamata wanawaomba pesa polisi karibia wote wana magari tena ya kifahari polisi wafate sheria na haki, na sasa tumejipanga kukutana na wasomi Dar es salaam ambao ni wazawa kutoka Tarime kuzungumza na kutoa kauli  kuhusu vitendo vibaya vinavyofanywa na polisi Tarime,Tarime isionekane kuwa ndiyo sehemu pekee ya hatari kuna mikoa mingine kama Kigoma inamatukio sasa hivi Tarime watu hawana uhuru wa kutembea hawana amani wanakamatwa ovyo"alisema.
 
Pia Heche amelaani vitendo vya mauwaji vinavyofanywa na polisi kwa kuwapiga kwa risasi na kisha kuachwa bila kulipwa fidia yakiwamo matibabu jambo ambalo linaifanya familia kuishi katika maisha magumu baada ya wanaowategemea kuuliwa na polisi wanaolinda  Mgodi pamoja na walinzi wa Mgodi wanao fahamika kwa jina maarufu Mobail.
 
Kwa upande wa Mwenyekiti vijana Wilaya ya Tarime Chacha heche  alisema kuwa tangu 2011-2012  watu wapatao 11 waeuwawa kwa kupigwa risasi Mgodini wakiwa na umri chini ya miaka 35 na kwamba hadi sasa  mahusiano kati ya polisi na raia yameshuka kwa kiasi kikubwa.
 
"kukamatwa kwa watu kwa kigezo kuwa wanapunguza uhalifu Nyamongo siyo suluhisho Serikali ilejeshe mahusiano mazuri baina yao na wananchi ,hakuna kikao chochote ambacho kimewahi kuwakutanisha polisi na raia kwa maana ya polisi jamii"alisema
 
Hata hivyo Mwenyekiti  vijana Taifa  ameiomba Serikali kuwatengenezea mazingira mazuri wananchi wa Nyamongo kwa kuwatengea maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo.
 
Kamanda wa polisi alipohojiwa na gazeti hili kuhusu tuhuma zinazowakabili polisi wake alisema kuwa swala la la polisi kuomba pesa ni mapungufu ya polisi mwenyewe kwani kazi ya polisi ni kukamata mtuhumiwa na kisha kumfikisha mahakamani ili mahakama ithibitishe tuhuma na si polisi kumtoza pesa mtuhumiwa ,nakwaba swala la oparesheni ni la Kitaifa ambapo kwa Tarime a lisema oparesheni ilistishwa Juni 23 mwaka huu.
 
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MWISHO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
 

No comments:

Post a Comment