MBARONI KWA KUJICHUKULIA SHERIA MIKONONI NA KUSABABISHA KIFO
Na. Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma
DODOMA JUMATANO
JULAI 18 2012. Jeshi
la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu watatu mbaroni kwa tuhuma za kujichukulia
sheria mikononi na kusababisha mauaji kwa mtuhumiwa wa wizi wa mifugo
aliyejulikana kwa jina la Juma Kidongoi,
mwenye umri wa miaka (36) Mgogo wa
Mugunga Wilaya ya Chamwino
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwanadamizi wa Jeshi la Polisi Bw. Zelothe Stephen
alisema watu hao walifanya tukio hilo la kijichukulia sheria mikononi siku ya
jumanne tarehe 17/07/2012 majira ya saa tisa na nusu alasiri katika kijiji cha Sejeli,
Kata ya Sejeli Tarafa ya Kongwa na Wilaya ya Kongwa.
Aliwataja watuhumiwa hao wa
kujichukulia sheria mikononi na kusababisha kifo kuwa ni Msafiri Matonya miaka
(27) Elikana Majimoto miaka (37) na Joel
Mazengo miaka (34) wote ni wakazi wa Kijiji cha Sejeli Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dododma
Akizungumzia tukio hilo Bw.
Zelothe Stephen alisema watuhumiwa hao
walimshambulia kwa mawe na fimbo mtuhumiwa wa wizi wa mifugo baada ya kujaribu
kukimbia wakati alipokamatwa na mgambo wakiswaga punda wa wizi kijijini hapo na kumsababishia kifo chake.
“Mgambo wa Kijiji cha
Sejeli walikuwa wamewakamata watuhumiwa watatu wa wizi wa mifugo, ghafla mmoja
wao akajaribu kukimbia ndipo wakapiga
mwano, na wanakijiji wakatoka kwa ajili ya ukamataji miongoni mwao wakiwa
watuhumiwa hao ambao walianza kumshambulia mtuhumumiwa huyo kwa mawe na fimbo.”
alieleza Kamanda Zelothe Stephen
Bw. Zelothe Stephen
alieleza kwamba watuhumiwa hao wa wizi
wa mifugo walikuwa wakiswaga Punda kumi na moja kati ya Punda hao kulikuwa na
Punda wanne mali ya Bw. Petro Chikumbi wa kijiji cha Banyibanyi kata ya Hogoro,
Kongwa ambao waiibwa katika mji wake mwingine huko katika kijiji cha Ngusele
wilaya ya Kiteto.
Kamanda Zelothe Stephen
alisema katika kuwatafuta punda hao ndipo mlalamikaji huyo alikutana na watu
watatu wakiwa wanaswaga punda kumi na moja katika kijiji cha Sejeli, Kwa kuwa
alikuwa peke yake aliogopa kuwauliza watu hao na badala yake akaenda kwa Afisa
Mtendaji wa Kijiji hicho kutoa taarifa.
Aidha Bw. Zelothe Stephen
alieleza kwamba Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Sejeli Bw. Maiko Machimo ailitisha
mgambo wa kijiji hicho na kuwaelekeza kwenda kuwafuatilia watu hao, ambapo
waliwakamata wakiwa na punda hao kumi na moja, ambapo mlalamikaji aliwagundua
punda wake wanne kwa alama alizowawekea katika masikio.
Katika utambuzi huo, ndipo
mmoja wa watuhumiwa wa wizi wa mifugo alijaribu kukimbia ambapo wanakijiji
walianza kumkimbiza mtuhumiwa huyo na kumkamata na kuanza kumshambulia kwa mawe
na fimbo mpaka akawa hoi na kumfikisha katika ofisi za Mtendaji ambako
alifariki dunia
Aidha Katika tukio hilo Kamanda
Zelothe aliwataja, watuhumiwa wawili wa wizi wa mifugo ambao wamekamatwa kuwa ni
Msafiri Chomola mwenye umri wa miaka (24) mgogo na makazi wa kijiji cha mugunga
katika wilaya ya Chamwino na Mtachi Kogani Miaka (38) mgogo wa Kijiji cha
Ng’inila kata ya Berege wilaya ya mpwapwa.
Mkuu huyo wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Dodoma alito wito kwa wanakijiji wa Sejeli kupitia mkakati wake
wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kuacha vitendo vya kujichukuilia sheria
mikononi na badala yake pindi wanapowakamata wahalifu wawafikishe sehemu husika
wakiwa salama ili kuruhusu upelelezi kufanyika kwa makini ili kuweza kubaini
mtandao wa uhalifu wa aina hiyo na kuutokomeza
katika maeneno yao.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment