MH MKONO ATIMIZA AHADI YAKE YA MADAWATI KWA SEKONDARI YA BUTUGURI
.Madawati yaliyotengenezwa na TASAF chini ya kiwango yarudishwa halamshauri ya Musoma
Mmilikiwa wa Blog ya Mwana wa Afrika akiwa diwani wa Kata ya Butuguri na waandishiwa habari katika shule ya sekondari Butuguri kushuhudia madawati mapya yaliyoletwa na Mh NimroDI Mkono Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Butuguri wakiwa katika moja ya darasa na kwenye madawati yaliyotengenezwa na Mh MkonoMwalimu akifundisha moja ya darasa lililotengenezwa na Mh Mkono
Shule inaendelea kama kawaida
Mwandishi wa ITV mkoani Mara akipata maelezo kutoka kwa Diwani wa Kata ya Butuguri Mh Mwita Charles
Baadhi ya Madawati yaliyotengenezwa na TASAF yakiwa yameharibika muda mfupi tangu yatengenezwe
Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Butuguri ( Geofrey Robert akihojiwa na Mwandishi wa ITV
Madawati ya TASAF
Madawati yaliyotengenezwa na Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Nimrodi Mkono
Madawati
Madawati mapya
Raha ya shule ni kusoma katika mazingira Bora
Madawati yaliyotengenezwa na TASAF yakipakiwa ndani ya gari tayari kurudishwa Halmashauri
Madawati chini ya kiwango yakipakiwa ndani ya gari kupelekwa TASAF
Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrodi Mkono akitazama baadhi ya madawati hivi karibuni na kubaini kuwa madawati hayo yaliyotengenezwa na TASAF kuonekana hayana kiwango
MUSOMA
MBUNGE wa
Jimbo la Musoma Vijijini Nimroadi Mkono amekamilisha ahadi yake ya kupeleka
Madawati mapya katika shule ya sekondari Butuguri baada ya kubainika kuwa madawati
yaliyotengenezwa na mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika shule hiyo hayana
ubora.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea awamu
ya kwanza ya Madawati zaidi ya 50,diwani wa kata ya Butuguri Mwita Charles alimpongeza
Mbunge huyo kwa kukamilisha ahadi hiyo huku
akitoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano huo.
Diwani huyo alisema kuwa Madawati yaliyotengenezwa
na TASAF hayana ubora na hivyo anaunga mkono kauli ya Mh Mbunge kuyarudisha Madawati
hayo katika Halmashauri ya Musoma.
Kuhusu wale wote waliohusika katika ubadhilifu huo
diwani huyo alisema kuwa wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria ili iwe
fundisho kwa viongozi wengine ambao wapo kwa masilahi yao.
Naye Mwalimu mkuu Wa Shule hiyo Godfrey Robert alisemshukuru
Mbunge huyo na kusema kuwa amesaidia kupunguza mzigo kwa wazazi katika
kukabiliana na upungufu wa madawati uliokuwepo shuleni hapo.
Amesema Madawati yaliyokuwepo hayatoshi ikilinganishwa
na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo,na hivyo mwaka huu walikuwa na mpango wa kutengeneza madawati
hayo.
Aidha madawati yote yaliyotengenezwa na mfuko wa
Maendeleo ya Jamii TASAF tayari yamerudishwa katika halmashauri ya Musoma
Vijijini kutokana na kutokuwa na kiwango kinachokubalika
Hivi karibuni akifanya ziara shuleni hapo mbunge wa
jimbo la Musoma Vijijini Nimrodi Mkono aliyakataa madawati zaidi ya 1000 yaliyotengenezwa
na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kutokana na kutokuwa na kiwango kinachokubaliwa



















No comments:
Post a Comment