Monday, July 9, 2012


       UKATILI WA KIJINSIA WADAU WATAKIWA KUPAMBANA NAO KATIKA JAMII

 Wadau wakiwa katika semina ya siku moja mjini Musoma mujadili suala la ukatili katika jamii
              Dr Grace Mallya kutoka wizara ya Afya akitoa elimu kuhusiana na suala la Ukatili
 Bi Martha Rimoy kutoka kitengo cha Afya ya uzazi na Mtoto akiwa katika semina hiyo
                            Wadau wakiwa katika semina hiyo
                                                   Wadau
        Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dr Samson Winani akiwa na Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mara ambaye ni mkuu wa wilaya ya Musoma Bw Jackson Msome
                                       Mkuu wa wilaya Bw Jackson Msome
                Picha ya Pamoja ya wadau waliokuwepo katika semina ya Ukatili wa kijinsia
                        Augustine Mgendi (Mwana wa Afrika)

                             Wawakilishi wa vyombo mbalimbali wakiwa katika semina hiyo
           
MUSOMA

VIONGOZI  MKOANI  MARA  WAMETAKIWA  KUSIMAMIA  SEKTA ZOTE ZINAHUSIKA  KATIKA KUPAMBANA  NA  UKATILI  WA  KIJINSIA  NA  KUHAKIKISHA  WAATHIRIKA  WANAPATA  HUDUMA ZOTE IKIWEMO  HAKI  YA  KISHERIA.

KAULI  HIYO  IMETOLEWA  NA  KAIMU MKUU MKOA WA MARA AMBAYE  NI MKUU  WA  WILAYA  YA  MUSOMA  JACKSON  MSOME  KWA  NIABA  YA MKUU  WA  MKOA  WA  MARA  KATIKA  MKUTANO  WA  SIKU  MOJA  KWA  WADAU WANAOPAMBANA NA  UKATILI  WA  KIJINSIA  UNAJADILI  MUONGOZO  WA  KISERA  NA  MUONGOZO  WA  KUTOA HUDUMA  KWA  WATU  WALIOATHIRIWA  N A UKATILI  WA KIJINSIA  KUTOKA  WIZARA  YA  AFYA UNAOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA UWEKEZAJI MJINI MUSOMA

AMESEMA SUALA LA UKATILI WA KIJINSIA NI SUALA MTAMBUKA AMBAPO JAMII INATAKIWA KUELIMISHWA JUU YA UKATILI HUO AMBAO UNASABABISHA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.

KAIMU MKUU WA MKOA HUYO AMESEMA KUWA MAKUNDI YOTE YANAYOPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA YANAPASWA  KUSHIRIKIANA NA SERIKALI IKIWA NI NJIA YA KUPAMBANA NA UKATILI HUO WA KIJINSIA KATIKA JAMII

NAYE MGANGA MKUU WA MKOA WA  MARA DK SAMSON WINANI AMESEMA KUWA  UKATILI WA KIJINSIA  HAUPO KWA WANAWAKE PEKEE BALI UKATILI HUO UPO MPAKA KWA WANAUME.

AWALI AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KATIKA MKUTANO HUO  MRATIBU WA KUZUIA NA KUPAMBANA NAUKATILI WA KIJINSIA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO MARTHA RIMOY AMESEMA KUWA  SUALA LA UKATILI WA KIJINSIA  NI SUALA AMBALO JAMII INATAKIWA KUPAMBANA NALO.

AMESEMA KUWA TANZANIA NI MOJA YA NCHI  ILIYORIDHIA MIKATABA MBALIMBALI IKIWEMO YA KUZUIA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA UKATILI DHIDI YA WATOTO AIDHA BI MARTHA RIMOY AMESEMA TANZANIA NI NCHI YA KWANZA KUFANYA UTAFITI WA KIKATILI DHIDI YA WATOTO HIVYO NI NJIA PEKEE YA JAMII KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA VITENDO HIVYO.

No comments:

Post a Comment