AENDA JERA MIAKA
20 KWA KUPATIKANA NA BUNDUKI SMG.
Dinna
Maningo,Tarime
MAHAKAMA ya
Wilaya ya Tarime Mkoani Mara imemuhukumu Mariba Chacha Kesabo mkazi wa Kijiji
cha Kangariani Kata ya Itiryo kwenda jera kifungo cha miaka 20 baada ya
kupatikana na Bunduki aina ya SMG na Risasi 14.
Akitoa hukumu
Hakimu Mkazi wa mahaka ya Wilaya ya Tarime Yusto Ruboroga alisema
kuwa kutokana na mahakama kusikiliza pande zote mbili Mahakama inamtia hatiani
Mariba Gesabo kwa makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni kupatikana na
Bunduki aina ya SMG yenye namba 052619 ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka 10
jera.
Kosa la pili ni
kupatikana na risasi 14 ambapo alihukumiwa pia kifungo cha miaka 10 nakwamba
adhabu zote mbili zinaenda kwa pamoja .
Upande wa
mashitaka ulipokea mashahidi 3,shahidi wa kwanza aitwaye Askari No.G 7055 D/C
James,Mwita Athumani ambaye ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Bilandi kijiji cha
Kangariani na shahidi wa tatu alikuwa ni Askari No. D8661 D/CPL Halson ambapo
upande wamshitakiwa hapakuwa na shahidi
Awali ilidaiwa
na mwendesha mashitaka wa polisi Sagent Abel Kazeni kuwa mnamo tarehe 3
Desemba 2011 majira ya saa 7 na nusu mchana alipatikana na hivyo vitu
nyumbani kwake akiwa amevificha kwenye shamba lake la migomba lililoko eneo la
nyumbani kwake.
Hata hivyo
mshitakiwa alijitetea kwamba bunduki hiyo alipewa na rafiki yake Marwa
Maico aishiye Nchini Kenya siku ya tarehe 28/7 2011 kwamba ataifata baadae
Mshitakiwa
alipopewa nafasi ya kujitetea ili apunguziwe adhabu baada ya kupatikana
na hatia hakusema chochote.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MWISHO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
AHUKUMIWA JERA
MWAKA MMOJA KWA WIZI WA GUNIA MBILI ZA MCHELE.
Dinna Maningo,Tarime
MAHAKAMA ya
Mwanzo Tarime Mjini Mkoani Mara imemuhukumu John Nyamanyi kwenda jera kifungo
cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa magunia mawili ya
mchele kila moja lenye ujazo wa zaidi ya kilo 80 ambapo anatakiwa kulipa
fidia ya kurejesha magunia hayo au pesa zenye thamani ya kiasi cha mchele pindi
atakapomaliza kutumikia kifungo.
Akitoa hukumu
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Jorome Mjini Tarime Migera alisema kuwa
Mahakama inamtia hatiani John Nyamanyi baada ya Mahakama katika kupitia
ushahidi wa pande zote Mahakama imeamini mshitakiwa ana hatia kwa kuiba mchele
sokoni kwani, baada ya kukamatwa mshitakiwa alidai ametumwa na Marwa
ambapo aliomba kwenda kumuita aliyemuagiza lakini hakuweza kurudi aliondoka moja
kwa moja nakwamba aliyedai kumtuma alikana kuwa hakumwagiza.
Alisema kuwa kwa
upande wa mashahidi 3 upande wa mlalamikaji walisema kuwa mnamo tarehe 17
mei 2012 mshitakiwa John Nyamanyi aliiba maginia 3 ya mchele yaliyokuwa
yamehifadhiwa chini ya uvungu wa meza ndani ya soko kuu la mjini Tarime ambayo
aliyatorosha majira ya saa 12 jioni ambapo hata hivyo gunia moja liliweza
kukamatwa na mlinzi wa soko wakati akijaribu kulitorosha na kuhifadhiwa kwa
mkuu wa soko.
Upande wa
utetezi ulileta shahidi mmoja ambaye ni mshitakiwa ambaye alieleza kuwa
aliagizwa na mwenzie aitwae Marwa ambapo alijitetea nakuomba kupunguziwa adhabu
kwa kuwa anafamilia na watoto wanaomtegemea.
Wazee washauri
Mahakama ya mwanzo Finias Asumi na Edward Maswi waliomba mshitakiwa
ahumkumiwe kifungo cha mwaka mmoja pamoja na kulipa fidia ya maguni 2 ya mchele
ili iwe fundisho kwa wengine ambapo Hakimu Migera aliunga mkono na hivyo
Mahakama kumtia hatiani kwa mujibu wa kifungu 265 na kanuni ya adhabu no.16 na
kumuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jera pamoja na faini ya kurejesha magunia
mawili ya mchele na kwamba haki ya rufaa iko wazi mbele ya mahakama ya Wilaya
ya Tarime.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MWISHO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment