MH MKONO KUTUMIA MILIONI 80 KUJENGA BARABARA ITAKAYOUNGANISHA TARAFA YA NYANJA NA MAKONGORO
WANANCHI
wa tarafa ya Makongoro,Nyanjkatika wilaya mpya ya Butima na baadhi ya vijiji
vya wilaya ya Bunda,wanatarajia kuondokana na tatizo kubwa la ukosefu wa soko
la mazao yao baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara itakayofungua
mawasiliano katika tarafa hizo.
Mh Mkono akicheza ngoma LITUNGU na wananchi wa eneo ambalo barabara inajengwa
Barabara hiyo ya changarawe inayojengwa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Mh Nimrod Mkono kwa gharama ya zaidi ya milioni 80 itawaondolea kero hiyo wananchi ambao kwa tangu uhuru wamekuwa wakilazimika kuuza mazao yao mashambani kutokana na ukosefu wa miundo ya barabara ya kusadia kufikisha mazao hayo katika soko.
Unapoaanzisha lazima ufuatilie kujua kama mambo yanaenda sawa
Mzee Ezra Okuta akimpongeza Mh Mkono kwa kuwajengea Barabara
Baadhi ya wananchi wa vijiji vinavyopitiwa na barabara hiyo mbali na kushukuru kwa hatua hiyo,wamesema tatizo la ukosefu wa barabara licha ya kuchangia kushindwa kufikia soko la mazao yao pia limechangia vifo vingi vya wananchi wakiwemo wanawake na watoto kwa kushindwa kufikishwa kwa wakati katika sehemu za matibabu.
Mwakilishi wa kituo cha ITV Mkoani Mara George Marato ambaye pia ni Mshauri wa Mbunge huyo katika masuala ya habari akifanya mahojiano katika ujenzi wa barabara hiyo na Mh Mkono
Ngoma ya LITUNGU ikanoga na George Marato akaingia kati kudumisha mila
Sehemu ya barabara ambayo bado hajaifikiwa kujengwa
Sehemu ya mazao ambayo yanaozea shambani kutokana na kutokuwepo na miundombinu ya kueleweka hasa barabara kufikisha mazao hayo sokoni
Kwa
upande wake Mh Mkono,amesema anasikitishwa na serikali kutumia mabilioni ya
shilingi kwa sherehe mbalimbali zikiwemo za uhuru huku wananchi wa vijijini
wakikabiliwa na matizo makubwa hasa ya ukosefu wa miundombinu ya barabaraba.
Barabara hiyo ni ya tano kujenga huku akitumia pesa yake mwenyewe katika jimbo la Musoma Vijijini
No comments:
Post a Comment