Wilaya
ya Bunda mkoani Mara inakabiliwa na mgogoro mkubwa ya ardhi jambo ambalo
linawafanya watendaji kutumia muda mwingi wa kazi katika kutatua changamoto
hizo.
Kauli hiyo
imetolewa katika kijiji cha Guta “B” na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Bunda Bw Cyprian Oyier wakati wa kukabidhi Hati za kimila 104 kwa
wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya mashamba 613 ambayo yamepimwa
kupitia mpango wa urasimishaji ardhi vijijini.
Amesema hivi
sasa karibu asilimia 90 ya changamoto za kila siku zinazoikabili halmashauri
hiyo ya Bunda ni migogoro ya ardhi hivyo kusema hatua hiyo ya kupimwa kwa
mashamba na wananchi kupatia hati miliki za kimila kutasadia kwa kiasi kikubwa
kupunguza migogoro hiyo.
Hata hivyo
mkurugenzi huyo wa halmashauri ya Bunda,amewaambia wananchi hao kuwa kupata kwa
hati hizo licha ya kusadia kutatua migogoro ya ardhi pia kutawawezesha kupata
mikopo katika vyombo mbalimbali vya fedha na hivyo kukabiliana na umasikini.
Kwa upande wake
meneja Urasimishaji ardhi Tanzania Bara kupitia mpango wa urasimishaji
rasmalimali na biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA,Bi Rehema
Ntimizi,amesema hadi sasa mpango huo umefikia halmashauri 34 nchini lengo
likiwa ni kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi katika mfumo wa kisheria na
kuitumia kuwaondolea umasikini.
Akizungumza kwa
niaba ya wananchi wa kijiji hicho,afisa mtendaji wa kijiji cha Guta “B” Bw
Raymond Misana,amesema changamoto kubwa ambayo imejitokeza wakati wa upimaji wa
ardhi ni pamoja na wananchi walio wengi kutoaamini kama hati hizo zinaweza
kuwasadia kupata mikopo katika taasisi za fedha huku wengine wakihusisha na
itikadi za kisiasa kwa kuhofu kunyang’nywa ardhi yao.
,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment