Wanafunzi washinda wakicheza katika maeneo ya shule
MUSOMA
HATIMAYE walimu wa shule za msingi
katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara,wameteleza mgomo ulitangazwa na chama cha
walimu Tanzania CWT katika kuishiniza serikali kuboresha maslahi yao na
mazingira ya kufanyia kazi.
Zaidi
ya shule 30 za msingi katika 44 na
sekondari 9 katika ya 18 katika Manispaa ya Musoma hazina walimu kuanzia leo asbuhi huku ofisi za nyingi za walimu na za walimu
wakuu zikiwa zimefungwa kwa makufuli.'
Aidha katika baadhi ya shule hizo licha ya kuwapo na wanafunzi lakini zikiwa na mwalimi
mmoja hasa mwalimu mkuu,ambao hawakuwa tayari kuzungumzia hali hiyo.
Baadhi ya walimu wamekizungumza kwa njia ya simu wakiwa
majumbani,wamesema wamelazimika kugoma baada ya kuridhishwa kuwa mgomo
huo umefuata taratibu zote za kisheria na kwamba wako tayari kwa lolote hadi
serikali itakapokubali kuboresha maslahi yao.
Taarifa kutoka wilaya ya Bunda,Serengeti,Butiama
zinasema hali ni hiyo hiyo huku wilayani Tarime licha ya walimu kugoma pia wanafunzi
wa shule maeneo ya mjini wamejipanga
katika bara bara kwaajili ya kufanya maandamano kwenda katika ofisi ya mkuu wa
wilaya ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono mgomo wa walimu wao.
Kutoka Tarime ,Dinna
Maningo
KATIKA hali
isiyo ya kawaida Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Msingi Wilayani Tarime
wameandamana hadi ofidi ya Ofisa elimu Wilaya ya Tarime Mkoani mara wakidai
haki zao za kupata elimu baada ya walimu wao kugoma kuingia madarasani na kisha
kuwataka wanafunzi kuondoka kwenda majumbani kwao .
Wanafunzi
hao walisikika wakiimba na kuongea mbele
ya Ofisa elimu wa Wilaya Emanuel Jonson katika viwanja vya ofisi ya elimu
Wilaya, walisema kuwa kitendo cha walimu kugoma kufundisha kinaathiri wanafunzi kwani kwa mgomo huo
wanafunzi walio wengi watamaliza shule bila kujua kusoma wala kuandika hivyo
wanaitaka Serikali kuwalipa walimu madai yao ili waendelee na masomo.
“Watoto
tunataka haki zetu, Watoto tunataka kupata
elimu, watoto tunataka kusoma tunaomba
walimu walipwe madai yao tuingie madarasani ,watoto tusinyimwe haki yetu ya
kupata elimu walimu wanapogoma waathirika ni sisi wanafunzi Serikali tatueni
mgomo wa walimu” walisema wanafunzi hao.
Ofisa elimu
Johnsoni aliwatuliza watoto hao na kuhaidi kutatua tatizo la walimu wao ambapo
aliwataka wanafunzi wote kurejea shuleni hapo kesho kuendelea na masomo yao.
Jonsoni
alisema kuwa anasikitika kwa kitendo cha walimu kutoingia madarasani na kwamba
kitendo hicho ni kupunguza stahili za watoto ambapo amewataka walimu wote kesho kuhudhulia
madarasani na kwamba ambao hawatohudhuria vipindi watawahibishwa .
“Kwa maelezo
ya Serikali mgomo ni batiri nimefanya kikao na waratibu elimu wote kuwaelekeza kwenda
katani kwao kuwahimiza walimu kurejea shuleni na kwa mujibu wa maelekezo
Serikali tumetoa taratibu za kujaza fomu kwa walimu wote za kuthibitisha
anaeunga mgomo au asiyeunga mgomo kwa wale ambao watagoma watachukuliwa hatua.”alisema
Jonson
“aliongeza”
Nasikitika walimu wamewafanyisha watoto
maandamano ,kugoma kunaathiri watoto walimu wasiwanyime watoto haki zao za
kupata elimu waendelee kufundisha wakati huo taratibu za Serikali zikifanyika, uzuri
kwa Wilaya yangu walimu hawadai madeni wanachodai ni posho,nyongeza ya mshahara,
na swala hilo ni la kitaifa Lingekuwa ni tatizo la kiwilaya ningetoa kauli
siwezi kutoa kauli tatizo ni la kitaifa”alisema Jonson.
Kuandamana
kwa wanafunzi hao ni baada ya walimu kutoka katika shule mbalimbali za msingi Wilayani Tarime kugoma
baada ya Serikali kushindwa kutekeleza mahitaji yao ya posho za
kufundishia,Nyongeza ya mshahara na posho za mazingira hatarishi ya kazi.
Mwenyekiti
wa chama Cha Walimu Wilayani Tarime Matinde Magabe alisema kuwa mgomo huo ni
endelevu hadi pale Mwenyekiti wa CWT Taifa atakapotoa tamko na kwamba hata
kesho hawatoingia darasani.
“Mgomo ni
halali tunataka Serikali itulipe nyongeza ya mshahara kwa asilimia 100%,posho
ya kufundishia asilimia 55 kwa walimu wa sayansi na hesabu asilimia 50 ya
mshahara kwa walimu wa masomo ya sanaa,posho ya mazingira magumu ya kazi asilimia
30% na mgomo huu ni endelevu”alisema Magabe .
Magabe
alisema kuwa Wilaya ya Tarime inajumla ya walimu wapatao 2870 kati yao ni wa
shule za msingi,Sekondari na walimu wa chuo cha walimu Tarime.
No comments:
Post a Comment