WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUFATILIA VYETI VYA KUZALIWA MAPEMA
Na Shomari Binda
Musoma,
Wazazi pamoja na walezi wametakiwa kuhakikisha wanafatilia vyeti vya
kuzaliwa vya watoto mapema baada ya kuzaliwa kama inavyoelekezwa na
kuacha tabia ya kuanza kufanya kazi ya kufatilia vyeti hivyo pale mtoto
anapotaka kwenda chuoni au kupata ufadhiri wa kwenda kusoma nje ya Nchi.
Hayo yamesemwa na Katibu tawala wa Wilaya ya Musoma Debora Makinga
alipokuwa akizungumza na BINDA NEWS juu ya kufatilia vyeti vya kuzaliwa
mapema na umuhimu wake kutokana na Wananchi wengi kutokuzingatia hilo
na baadae kuanza kuangaika pale wanapopata nafasi ya kufanya jambo
fulani.
Alisema kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na
msungamano wa Wananchi katika ofisi ya msajili wa vizazi,vifo na ndoa
wakifatilia vyeti vya kuzaliwa hususani kwa wale wanaotaka kwenda vyuoni
na kudai kuwa huo si utaratibu mzuri na unaweza kumfanya mtu kukosa
nafasi ya kwenda kusoma kutokana na kudharau kufatilia vyeti vya
kuzaliwa mara mtoto anapozaliwa.
Makinga alisema Wazazi
pamoja na walezi inabidi wabadilike na kuweka umuhimu wa pekee katika
suala la kupata vyeti vya kuzaliwa vya watoto mapema bada ya kuzaliwa
ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza pale litakapo hitajika
kufanyika jambo la msingi ambalo linahusu vyeti vya kuzaliwa.
"Hili nimekuwa nikilikumbusha mara kwa mara kupitia vyombo vya Habari
juu ya umuhimu wa kupata mapema vyeti vya kuzaliwa lakini bado Wazazi na
walezi wamekuwa hawazingatii na matokeo wanapokuja kufatilia na kukuta
kuna majukumu mengine ya kiutendaji wamekuwa wakilaumu ofisi",alisema
Makinga.
"Wapo wengine licha ya kuelewa umuhimu wa cheti cha
kuzaliwa wanashindwa kufatilia mapema na kuwa navyo na pale wanapopata
nafasi ya kazi ama kutaka kujiendeleza zaidi kielimu ndipo wanapoanza
zoezi la kufatilia cheti cha kuzaliwa,"aliongeza.
Alieleza
msongamano unaojitokeza kwa sasa katika ofisi yake kuhusiana na kutafuta
vyeti vya kuzaliwa umekuwa ukikwamisha kazi nyingine za kijamii na
hivyo kuwaomba Wananchi pale zinapokuwa zinafanyika kazi nyingine
wasilaumu bali wazingatie suala la kushughulikia suala la vyeti vya
watoto mapema mara baada ya kuzaliwa.
No comments:
Post a Comment