DC BUNDA AONGOZA HARAMBEE YA KWAYA.
Na Naomi Milton- Serengeti
Kanisa la menonite Tanzania limetakiwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupunguza umaskini na kuinua ubora wa maisha kwa watanzania.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya wa Bunda mh..Joshua Mirumbe alipokuwa akiongoza harambee ya kuchangia kwaya ya Upendo KMT Mugumu kanisa la menonite Tanzania wilayani Serengeti kwa ajili ya kutoa mkanda wa picha lengo ikiwa ni kutangaza injili.
Amesema uongozi uwe na malengo ya kuandaa ajira maalum kwa vijana kwa shughuli mbalimbali za kijamii mfano useremala,ushonaji,na uashi kwani hii itakuwa ni njia pekee itakayowasaidia vijana kujiendeleza kimaisha sambamba na mafunzo ya ufundi kwa vijana wote kila mkoa ili kupambana na suala la umaskin nchini
Kwa umuhimu wa kwaya ndani ya kanisa kuwa ni kuelimisha, kuburudisha na kuonya pia liwe na mtizamo mpana kuhusu ukosefu wa ajira kwa vijana si tatizo la Tanzania pekee bali ni dunia nzima.
Kwa Tanzania alisema tatizo hili linatokana na uchumi wetu kuwa mdogo kulinganisha na idadi ya watu waliopo kuwa kubwa.
.
Mapema akisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi kiongozi wa kwaya ya upendo .Bw.Jamuhuri Kabati alisema wameamua kufanya harambee kutokana na mapungufu waliyonayo ndani ya kwaya.
Tatizo kubwa walilolitaja ni uchakavu wa vyombo vya muziki kama vilekinanda,gitaa,mixer,na mike vilevile kuna tatizo la ajira kwa vijana kwani vijana wengi baada ya kujitosa kwenye uimbaji wanakosa pa
kuelekea.
Jumla ya tsh.9.320,000= zimepatiakana ikiwa ni pesa taslimu na ahadi kati yan hizo mgeni rasmi alitoa tsh,3,047,000=lengo lilikuwa ni kukusanya tsh,mil.10.
Mmoja wa waimbaji wa kwaya hiyo bi.Nezia Tanu amesema amefurahishwa na harambee hiyo kutokana na kiasi walichokipata kwani hawakutegemea kama fedha zote hizo zingepatikana kwa wakati huo.
Nae mchungaji wa kanisa hilo bw. Cleophace Nyamataga ametoa shukrani zake za dhati kwa mgeni rasmi na wote waliochangia kwaya yake kwa hali na mali kwani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza lengo lao nawamehaidi kutenda sawasawa na walivyokusudia.
No comments:
Post a Comment