WATU WANNE WASHILIKIWA KUHUSIANA NA UJAMBAZI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
Na Thomas Dominick,
Musoma
JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linawashikilia na kuwahoji watu wanne
wanaodaiwa kushirika katika tukio la ujambazi lililotokea June 20,
mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku Mivaro Campsite iliyopo katika Hifadi
ya Taifa ya Serengeti.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya
habari Mkoa hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Absalom Mwakyoma
alisema kuwa watuhumiwa hao walipatikana baada ya jeshi hlo kuendesha
oparasheni kabambe ambayo ilifanikiwa kuwakamata watu hao.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo ilisema kuwa majambazi wapatao nane walivamia
kambi hiyo ya watalii wakiwa bunduki na mapanga, na walipofika karibu na
sehemu ya kulia chakula walikutana na Meneja Msaidizi Renatus Robert
(42) ambapo walimfyatulia risasi kifuani na kuanguka chini akafariki
Dunia.
Baada ya hapo walikwenda kwenye hema namba 12 ambako
walikuwepo Mholanzi Erick Paul (58) na kumtaka atoe fedha Uero au dola
ambapo aliwaambia watoke ndipo walipompiga risasi ya paja na kumjeruhi
kwa mapanga mkono wa kulia na baadaye alifariki dunia kutokana na kuvuja
damu nyingi.
Kutokana na milio ya bunduki wananchi wa kijiji
cha Ikoma Robanda walielekea kwenye Kambi hilo kwa hamasa kubwa wakiwa
na silaha zao kila mmoja aliyoiona inamfaa, wahalifu hao baada ya
kusikia sauti zao hawakuendelea na oparasheni yao ya uhalifu wakatoweka
kwa kutumia gari walilokuwa wameliegesha porini.
Katika tukio
hilo iliwamlazimu wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki na
waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi kusitisha shughuli za
bunge na kufika eneo hilo na kutoa maelekezo yao juu ya kukomesha
matukio kama hayo yasijirudie pamoja na kuwataka wamiliki wa Makambi
ndani ya Hifadhi hiyo ya Taifa kuwa na walinzi wenye silaha.
Kamanda Mwakyoma alisema kuwa Jeshi hilo linaendelea na ufuatiliaji wa
wahalifu hao na kuwaomba wananchi wema kuendelea kushirikiana na Jeshi
la polisi kupata taarifa za wahalifu waliobakia ili kwa pamoja wapambane
na uhalifu.
No comments:
Post a Comment