MUSOMA
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, limeonya vikali kitendo cha
Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dk. Joyce Ndalichako cha
madai ya kuwafelisha wanafunzi wa kidato cha sita katika somo la maarifa
ya uislamu na kudai kuwa kitendo hicho ni hujuma dhidi ya uislamu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi
za Kiislamu Tanzania Sheikh Ramadhan Said Sanze,wakati akizindua
ushirika wa akiba na mikopo wa waislamu wa mji wa Musoma, unaojulikana
kama Kutayba SACCOS kwenye uwanja wa shule ya msingu ya Mkendo mjini
Musoma.
Sheikh Sanze, amewataka watu ambao wamehusika
kuwafelisha wanafunzi wa kiislamu katika somo lao la maarifa ya uislamu
kuacha kufanya hivyo, kwani matokeo ya hujuma hiyo yanaweza kusababisha
chuki, uhasama na matabaka miongoni mwa wananchi.
Kwa upande
Amiri Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Nchini Sheikh
Mussa Yusuf Kundecha, amewahimiza waislamu nchini kujiunga pamoja kwa
ajili ya ili kukopeshana bila riba ili kuboresha maisha yao.
Waumini zaidi ya 40 wa dini ya kiislamu mjini Musoma wamehitimu mafunzo
ya namna ya uendeshaji wa Saccos hiyo na kutunukiwa vyeti na zawadi
mbalimbali.
,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,
MUS0MA
SIKU chache baada ya Serikali kununua Kivuko kwaajili ya kutoa huduma
ya usafiri kati ya Manispaa ya Musoma na wilaya ya Rorya mkoani
Mara,kumeibuka mgogoro mkubwa ukihusisha vyama vya siasa vya CCM na
Chadema,huku viongozi wa CCM wilayani Rorya wakiandaa tamko litakalo
tolewa kwa Rais na Waziri wa ujenzi wakati wa uzinduzi rasmi wa safari
za kivuko hicho hivi karibuni.
Wakizungumza katika mkutano wa
halmashauri kuu ya CCM wilayani Rorya,baadhi ya wajumbe wa mkutano
huo,wamedai baada ya kivuko hicho kuwasili mjini Musoma,viongozi wa
Chadema wameonekana kukiteka kivuko hicho kwa kubadili Rangi na Jina
kutoka walilopendekeza la Mv Kinesi hadi kuitwa Mv Musoma.
Baadhi ya wajumbe hao Bi Filista Nyambaya na Bw Khalfani Msima,wamesema
kuwa kivuko hicho kiliombwa na wananchi wa wilaya ya Rorya lakini cha
kushangaza baada ya kuwasili tu kikiwa na rangi inayofanana na ile ya
bendera ya chadema kimeonekana kutekwa na kubadilishwa jina huku kilala
Musoma badara ya Kinesi wilayani Rorya.
Hata hivyo akizungumza
katika mkutano huo wa halmashauri kuu ya ccm,mbunge wa jimbo la Rorya
Mh Lameck Airo,amesema ingawa kivuko hicho kiliombwa na wananchi wa
jimbo la rorya kupitia kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Prof Phellemon
Sarungi,lakini si jambo la busara kuanzisha mgogoro bali hoja hiyo
wanapaswa kuiwasilisha kwa waziri mwenye dhamana siku ya uzinduzi rasmi
wa kivuko hicho.
Akizungumzia suala hilo meneja wakala wa
barabara Tanroads mkoani Mara,Mhadisi Emanuel Koroso,amesema rangi na
jina la kivuko hicho halijawekwa na chama chochote cha siasa hivyo
kuwaomba wananchi na wafuasi wa vyama hivyo kuachana na hoja kwani
amesema nia ya serikali kutatua tatizo la usafiri katika maeneo hayo
bila kujali chama cha siasa.
Serikali imenunua kivuko hicho
kwaajili ya kutoa huduma ya usafiri katika ziwa victoria kwa upande wa
wilaya ya rorya na musoma mjini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi
ya rais jakaya kikwete ya kuwaondolea shida wananchi wa pande hizo
mbili ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakisafiri kwa kutumia mitumbwi
na boti ambazo mara nyingi si salama.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,
RORYA
Wanawake wa kijiji cha Ikoma katika wilaya ya Roorya mkoani
Mara,wanalazimika kwenda kupata huduma za matibabu hasa za vipimo
mbalimbali vya uja uzito katika nchi jirani ya Kenya kutokana na kijiji
hicho kukosa zahanati tangu kuanzishwa kwake miaka 40 iliyopita.
Wanawake hao wametoa kilio hicho katika kijijini hapo katika mkutano wa
hadhara ambao umeitishwa na mbunge wa jimbo la Rorya Mh Lameck
Airo,kwaajili ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa
kijiji hicho.
Miongoni mwa wanawake hao Bi Monica Lucas na Bi
Bather Fabiani,wamesema kukosekana kwa zahanati katika kijiji hicho pia
kumechangia wanawake wengi kushindwa kupata huduma za vipimo kwa wakati
wote wa uja uzito hadi kujifungua na wakati mwingine kuchangia vifo kwa
wakina mama wajawazito.
Kufuatia kilio hicho,mbunge huyo Mh
Lameck Airo,amemteua mkandarasi kampuni ya Sirori Investment kuanza
haraka ujenzi kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la zahanati
lililopo kijijini hapo katika kuwandolea adha hiyo wananchi ambayo
inawafanya wanawake wajawazito na watoto kwenda kupata matibabu umbali
mrefu katika wilaya ya Tarime na wakati mwingine kuvuka mpaka hadi nchi
jirani ya Kenya.
No comments:
Post a Comment