Dinna Maningo,Mara.
JUMLA ya wahamiaji haramu na walowezi wapatao 319 wamekamatwa kwa kipindi cha
Januari hadi Mei Mwaka huu.
Akizungumza na Mwandishi wa habari ofisini kwake, Afisa Uhamiaji Mkoa
wa Mara, Jacob Sambai alisema kuwa kati ya hao wapo waliofikishwa mahamakani na
wapo waliorejeshwa kwao na wengine waliotumikia kifungo.
Alisema kuwa kati ya hao wapo Wakenya 259, Wathiopia 44,
Warundi 8,Wasomali 3, Waganda 3 na Wakongo 2.
Alisema kuwa hatua
zilizochukuliwa ni pamoja na kuwafukuza nchini ambapo waliofukuzwa ni watu wapatao
197 kutoka nchi mbalimbalimbali na wanaoendelea kuchunguzwa ni 39.
alisema kuwa waliokutwa
ni wakimbizi ni 8, waliofugwa kwa amri ya mahakama ni 9 na kwa wale ambao
kesi zao ziko mahakamani ni 7 ambapo waliogundulika ni watanzania kutokana
na mwingiliano na kufanana kwa lugha kati ya makabila ya Wakurya wa Kenya na
Wajaluo wa Kenya ni 9 na walioharalisha ukazi ni watu 60.
Sambai alisema kuwa Idara hiyo ina changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwa ni pamoja na uhalifu wanaofanyiwa wafanyakazi wawapo
kazini kuchomwa visu hadharani,Mauaji, uvamizi wa
kutumia silaha hali ambayo
inahatarisha maisha yao pamoja na tatizo la ubora na ufanisi wa kazi
jambo ambalo limewafanya watumishi kuwa na hofu kubwa ya kufanya kazi
huku wakihofia usalama wao.
“Kuna baadhi ya wenzetu si vizuri kuwataja majina yao
waliwahi kuvamiwa kwa kutumia silaha,kwa bahati njema walipona na wengine
kuchomwa visu wakiwa kazini,madhalani basi limekuja na abiria unawaambia
washuke ili wagongewe hati ya kusafiria passport, ghafla anakuja mtu
usiyemfahamu anakutaka vidole, mmoja wetu alifanyiwa hivyo, sasa hii ni hatari
sana” Alisema Sambai.
Alisema kuwa chagamoto zingine zinazoikabili Idara hiyo ni pamoja
na mwingiliano wa makabila kati ya
Wakenya wa kabila la Wajaluo na Wakenya wa kabila la Wakurya ambao wanafanana
tabia na Wakurya Watanzania na Wajaluo
wa Tanzania, kwa hiyo inakuwa ngumu kuwatofautisha na kuwatambua kutokana na
lugha zao kufanana na baadhi yao wamekuwa na mahusiano ya kindugu,pamoja na Uhaba
watumishi na ukosefu wa nyumba za watumishi imekuwa ikikwamisha ufanisi wa kazi kwenye idara hiyo.
Aidha kumekuwepo na baadhi ya viongozi wakiwemo wenyeviti wa
vijiji na baadhi viongozi wa vyama vya siasa hasa madiwani wamekuwa na asili ya
wakenya, hivyo inakuwa ngumu kumtaja mtu ambaye ameingia nchini na anaishi bila
kibali kutokana na mahusiano kati yao jambo ambalo limekuwa likikwamisha
utendaji kazi.
Aliongeza kuwa ukubwa wa mipaka umekuwa changamoto kubwa kwa idara hiyo
kutokana na urefu wake na umbali kwa vituo vya ukaguzi vya Kogaja na Shirati
kuwa nje ya mpaka nakwamba ni vyema ikahamishwa ili kuweka ufanisi wa kazi na
kufufuliwa kwa kituo cha Bolega
kilichoko Wilaya ya Tarime ambapo awali kilikuwa na msaada mkubwa.
Alisema kuwa kwa mwaka huu Idara ya Uhamiaji Mkoa huu imeweza
kutoa semina katika Tarafa zipatazo nane zenye kata 56 na vijiji au mitaa 210 katika
Wilaya za Bunda Tarafa ya Kikopya na Chamriho, Wilaya ya Rorya Tarafa ya Girango
na Tarafa ya Nyancha, Wilaya ya Serengeti
Tarafa ya Logolo na Gurument, Wilaya ya Tarime Tarafa ya Nyancha,vijiji vya Ichange
na Inchugu, Wilaya ya Musoma inatarajiwa kufanyika katika Tarafa ya Nyancha na
Makongoro.
Semina hizo zilikuwa na
lengo la kuweka ufanisi na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ambapo
namba za simu za viongozi zilitolewa kwao ili kutoa taarifa panapotokea mtu
ameingia nchini na anaishi bila kuwa na vibali.
Pia aliwasisitiza viongozi hao
kuwapa moyo wananchi kwani wamekuwa na uwoga wa kuwataja wahamiaji haramu
kutokana na kuhofia usalama wao wa kuhatarisha maisha.
No comments:
Post a Comment