WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS KIKWETE NCHIN ANGOLA
WAZIRI MKUU Mizengo
Pinda
WAZIRI MKUU Mizengo
Pinda anaondoka Dar es Salaam leo mchana (Alhamisi,
Mei 31, 2012) kwenda Luanda, Angola kuhudhuria
kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika
(SADC).
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Mkuu Pinda anahudhuria
mkutano huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambaye leo anatarajiwa kufungua
mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huko Arusha.
Mara baada ya kuwasili, leo jioni Waziri Mkuu atahudhuria kikao cha
TROIKA ambacho kinajumuisha Wakuu wa Nchi kitakachofanyika Ikulu ya nchi hiyo
na usiku atashiriki hafla maalum iliyoandaliwa kwa viongozi wakuu wa nchi za
SADC.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi za SADC ambao
umepangwa kufanyika kesho (Juni Mosi, 2012), utatanguliwa na mkutano wa
mawaziri unaoanza leo (Alhamisi, Mei 31, 2012) chini ya uenyekiti wa Waziri ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.
Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea jijini
nchini kesho kutwa (Jumamosi, Juni 2, 2012).
No comments:
Post a Comment