Dinna Maningo, Tarime.
MCHUNGAJI wa Kanisa la
Pentecostal Evangelistic Fellowship Africa(PEFA) Tawi la Gonsarara Kijiji cha
Kewanja Kata ya Kemambo-Nyamongo Wilayani Tarime Elia Magutu amewataka viongozi
wa Serikali kutumia hekima na kauli za busara pindi wanapohutubia wananchi
kupitia mikutano ya hadhara.
Kauli hiyo imekuja baada ya
mchungaji Magutu kudai kuwa hivi karibuni May 3 Mkuu wa Wilaya John
Henjewele akiwa anahutubia wananchi wa kitongoji cha Gonsarara kijiji cha
Kewanja alidaiwa kulikashifu kanisa na kusema kuwa kanisa la PEFA halipo
kihalali bali limeibuka na kuanzishwa kwa lengo la kufanyiwa tathimini ya
malipo katika zoezi linaloendeshwa na
mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaoendelea na tathimini kwa ajili ya
kuwahamisha wananchi wanaoishi jirani na mgodi wa dhahabu kitongoji cha
Gonsarara.
“Ilikuwa tarehe 3 May Mkuu wa Wilaya Henjewele akiwa katika
mkutano wa hadhara Gonsarara akiwa anazungumzia tathimini alisema kuwa kuna
watu wamekuja kutoka Mwanza na
kujenga nyumba ili nao wafanyiwe tathimini na mgodi wakati
anaendelea na maongezi alisema kuna Kanisa limeibuka la kitapeli lisilojulikana
na limetegeshwa ili nalo lifanyiwe tathimini ya malipo kauli hiyo ilitushangaza
kwa sababu katika hicho kitongoji kuna kanisa moja tu ambalo ni kanisa la
PEFA moja kwa moja ndilo alilokuwa
analilenga”alisema Magutu.
Mchungaji Magutu alikanusha
madai ya Mkuu wa Wilaya Henjewele la kuibuka kwa kanisa ambapo alisema kwa
kuonyesha vielelezo mbalimbali kuwa kanisa hilo lipo kwa muda mlefu tangu mwaka 1996 na
kwamba kauli hiyo ni kulizalalisha kanisa.
“Hili kanisa halijajengwa leo
limeanzishwa toka mwaka 1996 wakati huo tukiwa tunasali shuleni
Nyabigena-Kewanja ilipofika mwaka 2002 tukanunua eneo Gonsarara tukajenga
nyumba ya nyasi kulingana na uwezo mdogo tuliokuwa nao wakati huo tukaendelea
kusali likiwa linaongozwa na mzee wa kanisa aitwae Dishon Ghati baadae
tukajenga nyumba ya bati na sasa tunaendelea na ukarabati na kanisa ambalo hadi
sasa lina zaidi ya waumini 100”alisema Mchungaji.
Mchungaji huyo alisema kuwa
amesikitishwa na kauli hiyo ya Dc Henjewele na kumtaka aliombe radhi kanisa kwa
madai kuwa amelidhalalisha na kulikasfu hadharani bila kujua kwa undani
historia ya kanisa hilo
la PEFA.
“Kama Dc alikuwa na mashaka
na kanisa alipaswa afike kanisani aonane na uongozi wa kanisa tumweleze
historia ya kanisa siyo kuongea hadhalani kitu asichokijua,kanisa lipo kwenye
eneo halali tunamuomba achunguze kwa undani zaidi na hatuna sababu yoyote ya
kuhamishwa na wala hatujaomba mgodi utuamishe kama mgodi umeona kanisa lipo
jirani na mgodi na kunahaja ya kuamishwa kwa shuguli zao ni maamuzi yao
wenyewe”alisema
Aliongeza” Sisis hatuna
taarifa yoyote wala barua kuwa mgodi unataka kufanya tathimini kanisa na
kuliamisha na itambulike kuwa kanisa la PEFA
ni taasisi inayotambulika lina haki ya kujiendesha kikanisa,kuboreshwa
kwa kanisa Dc anasema tunafanya hivyo kwa ajili ya malipo ya kuhamishwa! Je
toka tathimini imeanza ni kanisa lipi ambalo limefanyiwa tathimini? Hakuna.
Mchungaji Magutu alisema kuwa
kutokana na kauli ya Dc Henjewele huwenda ikaathili waumini kwa kudhani kuwa halikuwa kanisa bali lipo
kwa ajili ya kutafuta masalahi binafsi ambapo pia aliwataka waumini kuendelea
kusali na kumtumikia Mungu nakwamba wasikatishwe tamaa na kauli ya Henjewele.
Mwenyekiti wa kanisa la PEFA
Wilaya ya Mashariki Tarime Mchungaji Samson Msabi alithibitisha kuwepo kwa
uhalali wa kanisa hilo
ambapo alisema aliliweka wakfu mwaka 2008.
Pia Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kewanja ambako ndiko kuliko na kanisa hilo
Tanzania Omtima( Chadema) alithibitisha kuwepo kwa kanisa ambapo alisema
analitambua kutokana na kuwepo kijijini kwake kwa muda mlefu.
Mkuu Wa Wilaya ya Tarime John
Henjewele alipoelezwa tuhuma hizo dhidi yake alikili kuwepo kwa kanisa hilo
nakusema siyo kanisa halali nakwamba
limeibuka na kutegeshwa kwa lengo la kufanyiwa tathimini na mgodi na kwamba
ameliona hilo kanisa kwa macho yake ambalo alisema halijui jina la kanisa
kwakuwa kanisa hilo halijaandikwa jina.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MWISHO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment