TUDUMISHE MUUNGANO WETU
Habari wana wa Afrika,Habari Tanzania,nikiwa kama mmilikiwa blog ya Mwana wa Afrika napenda kuchukua nafasi kuwapongeza Watanzania wote katika kusherekea Miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,si kazi ndogo kudumisha Muungano wetu mpaka kufikia hatua hiyo kwani tumeshuhudia nchi nyingi duniani zinashindwa kuheshimu muungano wanaokuwa nao na kuamua kuuvunja lakini kwetu TUMESHINDA, Eeeeeh Asante Mungu
Pamoja na hayo na mambo mengi katika Muungano wetu bado kuna baadhi ya watanzania wanamtazamo tofauti katika Muungano huo kutokana na kile kinachosemekana baadhi ya sehemu kutonufaika na muunngano huo.
Katika Muungano wetun kuna mambo mengi ambayo Viongozi wetu walikubaliana kuwa kama sehemu ya Muungano kitu ambacho ni kizuri na cha kupongezwa,baadhi ya sehemu hizo ni kama Mambo ya nje,Jeshi,Polisi,Mamlaka ya dharura,Uraia,Uhamiaji,Biashara ya nje,Utumishi wa umma,Kodi ya mapato, orodha,Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu.
Hayo ni mambo mengi na ambayo kwa pamoja viongozi wetu waliamua kwa kauli moja kusema kuwa tushirikiana katika hayo,napenda kuchukua nafasi hii kama mtanzania halisi,mtiifu na mzalendo kwa nchi yangu kusema kuwa muda umefika Viongozi wetu wamalize tatizo ambalo linaonekana kuwepo kwenye suala la Muungano
Napenda kutoa pongezi kwa Rais mstaafu wa Zanzibar Aman Abed Karume kwa Amani aliyoiacha Zanzibar kwa ushirikiano mkubwa na Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUfMaalim Self Sharff Hamad,naweza kusema hali iliyokuwepo Zanzibar kabla ya maridhiano ilikuwa inatia shaka katika Muungano wetu
Rai yangu kwa viongozi Muungano ni urithi pekee ambao wazee wetu Mwl Julius Nyerere na Mzee Abed Aman Karume wametuachia hivyo hatuna budi kuuenzi kwa mikono miwili,ili tuuenzi Muungano huo lazima viongozi wawasikilize wananchi nn wanasema juu ya Muungano wao na je wanataka uwe vp ili tuendelee kuudumisha.
Pamoja na hivyo pia ni vyema viongozi wakatathimini Raslimali za nchi zinawanufaisha nchi wote wa Bara na Visiwani,naamini kama tutaondoa kero hizo bila shaka Muungano wetu utakuwa wa mfano Duniani.Yapo mengi ila tuanzie hapo kwa leo
Augustine Mgendi
Mwana wa Afrika
Wako katika Kudumisha Muungano wetu
No comments:
Post a Comment