Tarime.
BAADHI ya Wazazi wa Wanafunzi
wanaosoma Shule ya Msingi Kiongera Kata ya Susuni Wilaya ya Tarime Mkoani Mara
wameulalamikia uongozi wa shule hiyo kuwatumikisha Wanafunzi kufanya kazi
mbalimbali za walimu.
Wakiogea na gazeti hili
walisema kuwa Wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakifanyishwa kazi nzito za
shamba pamoja na kuagizwa vitu mbalimbali kwa maslahi ya walimu.
“Wanafunzi wanafanyishwa kazi
kiasi kwamba hata kupata ile nafasi ya
kujisomea inakosekana sasa hivi ni
kipindi cha palizi za mashamba watoto wanaenda kupalilia mashamba ya walimu
wanalima toka asubuhi hadi saa nne”alisema Joice Bhoke.
Chacha Mwita alisema kuwa
mbali na wanafunzi hao kupariria mashamba ya walimu pia wamekuwa wakivuna mazao
nyakati za mavuno hali ambayo inawafanya kuichukia shule na wengine kutoroka
shuleni.
“Wanafunzi wamegeuzwa vibarua
mazao yakikomaa wao ndio wavunaji wanavuna mahindi wanabeba toka mashambani wanapukuchuwa mtoto
anafika nyumbani vidole vinauma kama
kipindi mashamba yamebana watoto wanafanyishwa kazi kama
punda akifika nyumbani unamwonea huruma inabidi apumzishwe na kazi za nyumbani
kutokana na uchovu”alisema Mwita.
Wazazi hao walisema watoto
hao wamediriki hata kuwatekea maji walimu ambapo pia wamekuwa wakiagizwa
kupeleka kuni,fito za kujengea majiko au kuzibia uzio wa nyumba na mashamba yao.
“Watoto wanafundishwa kazi
nzito wakati huo huo wanaagizwa vitu mbalimbali mtoto huyo huyo unamkuta
amebeba Jembe,wakati huo huo ana galoni limejaa maji,ana Panga,hapo hapo
amebeba Madaftari analemewa na mizigo akifika shuleni anakuwa hoi watoto
wengine wanatoka umbali mlefu bado anatakiwa aingie darasani kusoma wakati huo
bado anatakiwa kufanya shughuli za shule na za walimu za kuwasombea maji
visimani,Nyumbani kazi zinamsubiri yeye kama unavyojuwa maisha ya vijijini
tukiwazuia walimu hawafundishi na tatizo hili ni kwa shule zote za hapa katani “alisema
Nchimbya Muhoni.
Pia Shule ya msingi
Kikomori,Nyabirongo na Matamankwa zilizopo katika kata hiyo ya Susuni ni
miongoni mwa shule zinazodaiwa wanafunzi kutumikishwa na walimu.
Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kiongera Lucas Kisairo alipoelezwa tatizo hilo
la wanafunzi kufanyishwa kazi alisema
kuwa wananchi kupitia mkutano mkuu walihiari wanafunzi kupelekea walimu kuni na
mahitaji mengine kama njia ya kujenga nao
mahusiano na kwamba wanawasaidia kuwaboreshea maisha.
Mkuu wa shule hiyo ya msingi
Kiongera Daniel Machera alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa hakuna mwanafunzi
yoyote anayefanyishwa shughuli za shamba na kwamba kuhusu wanafunzi kupelekea
walimu kuni ni makubaliano ya wazazi na
kwamba wanamihitasari ya makubaliano ya wanafunzi kuwapelekea kuni za kupikia
na kuwatekea maji.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MWISHO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment