Wednesday, April 18, 2012

SINGIDA.

KAMPUNI YA KIHELYA AUTO TRACTOR PARTS LTD, INAYOJISHUGHULISHA NA UUZAJI WA MATREKTA KWA WAKULIMA WADOGO WADOGO WAKIWEMO WANACHAMA WA VYAMA VYA USHIRIKA (SACCOS), NCHINI, IMEKABIDHI MATREKTA MANNE YA MKOPO KWA WANACHAMA WA UKOMBOZI ULEMO SACCOS MKOANI SINGIDA, YENYE THAMANI YA SH. MILIONI 226 IKIWA NI KUWAWEZESHA KUANZISHA KILIMO CHA KISASA, MAARUFU 'KILIMO KWANZA'.

MATREKTA HAYO AINA YA MASSEY FERGUSON YAMEKABIDHIWA JANAI NA KAIMU MKUU WA WILAYA YA IRAMBA, BW. EDWIN ABEL SHIJANGA KWA WANACHAMA HAO WA UKOMBOZI ULEMO SACCOS, KATIKA HAFLA FUPI ILIYOFANYIKA KWENYE OFISI ZA SACCOS HIYO ZILIZOPO KATA YA ULEMO-MISIGIRI MKOANI SINGIDA.

AKIZUNGUMZA KATIKA HAFLA HIYO ILIYOHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA VYAMA NA SERIKALI, KAIMU MKUU HUYO WA WILAYA YA IRAMBA, BW. SHIJANGA AMEELEZA KUFURAHISHWA NA HATUA HIYO NZURI ILIYOFIKIWA NA WANACHAMA WA ULEMO SACCOS KATIKA KUNUNUA MATREKTA HAYO JAPO KWA MKOPO KUPITIA BENKI YA TIB.

AMESEMA, KILIMO CHA KISASA KINATAKIWA KUPEWA UZITO WA HALI YA JUU ILI KUWAWEZESHA WATANZANIA KUPATA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIMAENDELEO, NA KWAMBA WAKATI UMEFIKA SASA KWA JAMII YOTE KUJIKITA ZAIDI KATIKA KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA KISASA, KWA KUCHUKUWA MIKOPO YA MATREKTA YANAYOUZWA NA KAMPUNI HIYO YA KIHELYA ILIYOPEWA DHAMANA NA SERIKALI KUU.

AIDHA, KAIMU MKUU HUYO WA WILAYA AMEUPONGEZA UONGOZI WA KAMPUNI HIYO YA KIHELYA AUTO TRACTOR PARTS LTD, CHINI YA MKURUGENZI WAKE, BW. LAZALO KIHELYA KWA USHIRIKIANO WAKE MZURI NA SERIKALI, KATIKA KUTIMIZA AZMA HIYO YA KUWAKOPESHA MATREKTA WAKULIMA WADOGO NA WANACHAMA WA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI.

AMEWATAKA WATANZANIA WOTE WANAOHITAJI KUPATA MIKOPO YA ZANA HIZO ZA KILIMO KUHAKIKISHA WANAFUATA TARATIBU NA MASHARTI YALIYOWEKWA NA SERIKALI KUPITIA BENKI YA TIB NA TAASISI YA KUWAWEZESHA WAKULIMA ZANA ZA KILIMO (PASS), NA KWAMBA MARA BAADA YA KUKAMILISHA MASHARTI HAYO KAMPUNI HIYO YA KIHELYA ITAWAKOPESHA MATREKTA KWA MUJIBU WA SHERIA.

KWA UPANDE WAKE, WAKALA WA KAMPUNI YA KIHELYA MKOANI SINGIDA AMBAYE PIA MWENYEKITI WA MUUNGANO WA ASASI ZA KILIMO, BW. JUMA MENE AMESEMA, JAMII YA KITANZANIA INATAKIWA KUJIUNGA NA VYAMA VYA SACCOS ILI KUPATA MIKOPO KAMA HIYO YA MATREKTA KUTOKA KAMPUNI YA KIHELYA.

AKITOA SHUKRANI KWA NIABA YA WAKULIMA WENZAKE WALIOKOPESHWA MATREKTA HAYO, MWENYEKITI WA UKOMBOZI ULEMO SACCOS, BW. JONAS ABEL MPONDA AMESEMA KWAMBA, MATREKTA HAYO WATAYATUMIA VIZURI SANA KATIKA KUENDELEZA KILIMO CHA KISASA NDANI YA WILAYA NA MKOA HUO, ILI KUFIKIA MALENGO YAO YA KUPIGA VITA UMASIKINI WA VIPATO.


No comments:

Post a Comment