MWENYEKITI WA MTAA AJIUZULU NA KUHAMIA CHADEMA
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wimbi
la Wenyeviti wa Mitaa kujuzulu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), na
kuhamia CHADEMA limeingia katika sura mpya, baada ya Mwenyekiti wa Mtaa
wa Ilolo Kati Bwana Ngambi K Ngambi naye kujiuzulu.
Tukio
hilo limetokea Aprili 24 mwaka huu katika Mkutano wa hadhara
uliofanyika katika mtaa huo na kuhudhuriwa na baadhi ya madiwani wa
CHADEMA jijini Mbeya wakiwemo madiwani wa Kata za Mwakibete, Forest,
Sinde ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Akifungua
mkutano huo Diwani wa Kata ya Sinde Mheshimiwa Fanuel Kyanula, alitoa
taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Sinde ambapo
kila mwananchi alikuwa akichangia shilingi 3,000 badala ya shilingi
10,000 za awali.
Aidha
mchango huo umesaidia kumalizia kabisa ujenzi wa madarasa hayo,
amewashukuru wananchi kwa kuitikia wito wa kuchangia mchango huo bila
usumbufu na kipingamizi cochote.
Diwani
Kyanula akielezea matumizi ya mchango huo umeweza kukidhi kazi ya
upigaji wa sakafu na uwekaji wa nyaya za umeme, hatua hiyo ambayo
Mkurugenzi wa Halmashauri alitoa pongezi kwa na usimamizi mzuri hadi
kufikia kukamilika kwa ujenzi huo.
Naye
Diwani wa Kata ya Mwakibete Bwana Lucas Mwampiki amempongeza mwenyekiti
huyo wa mtaa Bwana Ngambi na kwamba ni kiongozi mchapa kazi, hodari na
hivyo wao kwa sasa wamempata Kamanda ambaye ataongoza mapambano dhidi ya
ubadhilifu.
Kwa
upande wake Bwana Gambi amesema kujiunga kwake CHADEMA ni hiari yake na
wala hajalazimishwa na mtu bali ni kuchoshwa ba ukandamizaji ambavyo
vilikuwa vikifanywa na CCM naye kwa kuwaonea huruma wananchi aliokuwa
akiwaongoza.
Katika
mkutano huo watu kadhaa walikabidha Kadi za CCM wakiwemo Rose
Mwashilindi (50), Atusekelege Asumbisye (52), ambaye alikuwa balozi wa
mtaa huo na Samson Mwakibole.
Katika
hadhara hiyo Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya Bwana John
Mwambigijaaliwapongeza waliohamia kwa hiari yao kujiunga na Chama hicho
na kudai kina watu makini ndio maana kimekua kikipata mafanikio siku
hadi siku na kutamba 2015 wataichukua dola.
Kuhama
kwa Ngwambi aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Ilemi ni pigo kubwa kwa CCM
kwa kipindi cha hivi karibuni kwani Mwenyekiti wa mtaa wa Ilemi Bwana
James Joseph Mbela naye alihamia CHADEMA akidia amechoshwa na ufisadi
uliokithiri ndani ya CCM.
No comments:
Post a Comment