KAMATI ZA MAAMUZI ZA
VIJIJI ZISIINGILIWE KWENYE MAJUKUMU YAKE
.
Dinna Maningo,Tarime
WENYEVITI wa Vitongoji,Vijiji
na Watendaji wa Vijiji na Kata katika kata ya Bumera Wilayani Tarime Mkoani
Mara wamedaiwa kuchangia kuwepo kwa migogoro ya Ardhi kutokana nakuwa wamekuwa
wakihusika kufanya maamuzi ya uuzaji na
ugawaji wa ardhi kinyume cha sheria.
Hayo yalibainishwa na
wananchi wa kata ya Bumera kutoka kijiji cha Turugeti,Kitenga na Kwisarara
wakati wakipatiwa Semina ya mafunzo ya udhibiti wa migogoro ya ardhi
yanayoendeshwa na kituo cha Sheria na haki za Binadamu Tarime (SHEHABITA) kwa
ufadhili wa Foundation for Civil Society,yaliyofanyika katika ofisi ya Kata ya
Bumera iliyopo kijiji cha Kitenga.
Wananchi hao walisema kuwa
kumekuwa na tabia ya Wenyeviti,na Watendaji kuingilia kazi za kamati ya maamuzi
za vijiji wakati wa maamuzi ya migogoro ya ardhi.
“Kuwepo kwa migogoro ya ardhi
kunatokana na hawa Wenyeviti, na Watendaji kujichukulia maamuzi wao wenyewe
ndiyo uhusika kuuza na kugawa ardhi matokeo yake wanashindwa kusuluhisha
migogoro Wenyeviti ni mahodari wa kugawa ardhi”alisema Lucus Chacha mkazi wa
Turugeti.
Josephu Magaigwa Mkazi wa
kijiji cha Kitenga alisema tatizo
lingine linalochangia kuwepo kwa mgogoro wa ardhi Bumera unatokana na Kamati ya
Fedha, Mipango na Uchumi za Kijiji kuwa ndiyo wagawaji wa ardhi.
Pia walisema kutokuwepo kwa mipaka ya haki ya njia imechangia
mgogoro na kuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana na baadhi ya watu wamekuwa
wakiziba njia hali inayosababisha usumbufu kwa watu na mifugo inayokwenda
malishoni.
“Kuna mgogoro mwingine wa
ardhi ambayo ni njia kumekuwa na tabia
ya baadhi ya watu kuziba njia kwenye makazi yao watu wanakosa mahali pa
kupita na hata kupitisha mifugo yao inaleta usumbufu tunazunguka mbali nawakati
kuna njia halali za mkato ambazo zimezibwa na unapomwambia mtu azibuwe inakuwa
ni mgogoro mkubwa”alisema Nyamuhanga
Kisiri mkazi wa Kwisarara.
Rhobi Wambura mkazi wa Kijiji
cha Turugeti alisema kuna watu walihamishwa
kwenye makazi yao
wakati wa oparesheni vijiji mwaka 1974 ambapo imesababisha kuwepo na tatizo la
kugombea eneo na hivyo kusababisha migogoro ya ardhi.
‘Kuna watu walihamishwa
kwenye makazi yao
wakati wa oparesheni vijiji wakaondoka
baadae ardhi walizoziacha zikakaliwa na watu wengine watu wameishi
kwenye maeneo hayo zaidi ya miaka 15 leo hii wale waliohamishwa wamerudi na
kudai ardhi kuwa ni ya wazee wao hali inayoleta mgogoro alisema Rhob Wambura.
Anaongeza” Kibaya zaidi kuna
mgogoro mwingine kuna mkazi mmoja aishiye Tarime mjini alihama Turugeti kitambo
eneo likabaki wazi akahamia mtu mmoj kipindi cha oparesheni vijiji ameishi
zaidi ya niaka 15 leo hii anaambiwa na Mahakama ya Ardhi na Nyumba Wilaya ya
Tarime aondoke kwenye eneo kapewa siku tano awe amehama yeye na familia yake
aondoke aende wapi na anafamilia! Unafikili kinachofata ni nini ? nimapigano
kwa sababu ametafuta haki yake hadi mahakama ya ardhi ya nyumba wilayani
imekosekana anaambiwa anatakiwa kuachia eneo”alisema
Kwa upande wa wajumbe wa
kamati ya maamuzi ya vijiji walisema kutokana
na kutofahamu sheria wameshindwa kuwajibika katika uamuzi wa migogoro kutokana
na kutojuwa aamajukumu yao ya kazi jambo ambalo limepelekea Halmashauri za
kijiji kutekeleza majukumu yasiyo yao kwa kile wanachoamini wenyeviti na
Watendaji ndiyo wahusika pekee katika utatuzi na ugawaji wa ardhi.
Bonny Matto ambaye ni
mkufunzi wa mafunzo aliwataka viongozi wa Serikali za Vijiji kuacha tabia ya
kugawa na kuuza ardhi bila ridhaa ya wananchi huku akiwasisitiza wananchi
kuacha tabia ya kuuza ardhi bila kushirikisha Halimashauri za kijiji ambayo imekuwa
ikisababisha kugombea ardhi na
kusababisha mapigano ambapo alikazia kuwa tabia ya kupigana kwa kukatana mapanga
si njia sahihi ya kutatuwa migogoro.
“Kwanini watu wakatane
mapanga kwa sababu ya ardhi je toka watu wapigane wamenufaika na nini? Hakuna
manufaa yoyote matokeo yake watu wanamwaga damu wanakufa na kuacha familia
zikiishi kwa mateso,njia pekee ni ya usuluhishi wa matatizo ni vyombo vya
utatuzi wa migogoro ya ardhi kuna mabaraza ya ardhi ya kijiji,mabaraza ya kata,
mahakama ya ardhi na Nyumba wilaya,Mahakama kuu na mahakama ya Rufaa nendeni
huko mkatapate haki zenu.
Anaongeza” hili tatizo la
mipaka ya njia ni kazi ya kamati ya maamuzi ya kijiji wao ndiyo wanatakiwa
kuweka mipaka wanapoweka mipaka wanatakiwa kuacha haki ya njia,haya matatizo
yanakuwepo kwa sababu ya kuuziana ardhi kiholela bila utaratibu Halmashauri za
kijiji zifuate taratibu za kisheria na wawajibike kwa nafasi zao wasikumbatie
madaraka yote wagawane madaraka mgogoro wa ardhi utakoma pia kisheria mtu
anapoishi kwenye eneo zaidi ya miaka 12 ardhi hiyo ni halali hapaswi
kunyang’anywa na mtu yeyeote akifanya hivyo amevunja sheria ya ardhi ya vijiji
No 5 ya mwaka 1999.alisema Matto.
Kabla ya kuanzishwa kwa mkoa
wa kipolisi Tarime/Rorya Kata ya Bumera ni miongoni mwa Kata zilizokubuhu kwa
migogoro ya ardhi iliyosababisha mapigano ya koo baina ya koo ya Wamera na
Wahunyaga,Wamera na Wajaruo,Wahunyaga na Wasweta,ambapo sababu ya mapigano ni
kutokuwepo kwa mipaka halisi baina ya kijiji na kijiji ambapo mpaka sasa
serikali bado haijabainisha mipaka halisi ikiwemo mipaka ya haki ya njia
inayoendelea kusababisha migogoro ya ardhi.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MWISHO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment