Saturday, April 21, 2012

HAUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JERA KWA UBAKAJI,NA MIAKA 5 KWA WIZI.
Dinna Maningo,Tarime.

MAHAKAMA ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara imemuhukumu Kanisiusi Mwita (24) Mkazi wa Tarime kifungo cha maisha jera kwa kosa la ubakaji na kifungo cha miaka 5 kwa wizi.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime Odira Amworo alisema kutokana na makosa mawili aliyotenda mahakama inamuhukumu Kanisiusi Mwita kwenda jera kutumikia kifungo cha maisha kwa kosa la ubakaji pamoja kifungo cha miaka 5 kwa wizi ambapo pia anatakiwa kulipa fidia ya sh milioni 2 kwa mlalamikaji kwa kumsababishia maumivi.

Mwendesha mashitaka wa polisi Casimiri Kiria alisema kuwa mshitakiwa mnamo tarehe 22 septemba mwaka jana majira ya saa 6 mchana eneo la Gamasara kata ya nyandoto mtuhumiwa akiwa ndani ya gari akiwa anamtishia kwa kisu alimbaka binti wa miaka 14 Hellena Kisagero mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Nkende mwaka jana.

Pia alisema  mshitakiwa aliweza kuiba  viatu vyake,nguo za shule,pesa,na jumla ya thamani ya vitu vyote ni sh. elfu 69,000 ambapo kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani mnamo septemba 26 mwaka jana  akituhumiwa na makosa mawili ya ubakaji na wizi.

Kiria alisema mlalamikaji akiwa eneo la Seng'esa alimwomba lifti ya gari mshitakiwa na kumtaka amshushe kibao cha shule lakini yeye alimpitiliza hadi kijiji cha Gamasala eneo la vichakana na kumbaka huku akiwa anamtishia kumchoma kisu.

Alisema mshitakiwa alikuwa anafanya kitendo hicho cha ubakaji ndani ya gari ambapo mlalamikaji alipiga yowe na kusababisha wananchi kufika eneo la tukio na kupiga simu polisi na hivyo mshitakiwa aliweza kukamatwa na kufikishwa mahakamani

Kwa upande wa mashahidi upande wa mashitaka walikuwa 8,mshitakiwa akiwa hatiani alipewa nafasi ya kujitetea ambapo alijitetea kuwa hakutenda makosa.

                                                 ,,,,,MIWSHO,,,,,

No comments:

Post a Comment