HUKUMU YA TINDU LISU LEO
KESI
inayomkabili mbunge wa Singida mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu
Lissu, iliyofunguliwa mjini Singida kupinga ushindi uliomweka
madarakani, itatolewa kesho ijumaa (Aprili 27, mwaka huu).
Hukumu
itatolewa na Jaji Moses Mzuna, anayesikiliza kesi hiyo, iliyofunguliwa
na makada wawili wa CCM, Shabani Itambu na Pascal Hallu.
Kesi
hiyo imekuwa kivutio sana kwa wananchi wengi wa mkoa Singida na nchini
kwa ujumla, kutokana na umaarufu wa mbunge huyo machachari.
Jaji anayesikilia shauri hilo mjini Singida, anatoka mahakama kuu kanda ya Kilimanjaro.
Walalamikaji
wa kesi hiyo, iliyofunguliwa mahakama kuu kanda ya Ddoma,
wanatetewa na wakili Godfrey Wasonga, kjtoka mkoani Dodoma, na Lissu
amejisimamia mwenyewe.
Kesi
hiyo ilianza kusikilizwa Machi 12, 2012, kufuatia makada wawili wa
CCM, kupinga ushindi wa Lissu kwa madai kuwa uchaguzi huo uligubikwa
na dosari nyingi.
Katika
mahojiano na Lissu, amesema vyovyote mahakama itakavyo
hukumu, anajivunia kuimarisha demokrasia na kuwa mbunge wa kwanza
kutoka upinzani, kwenye historia ya mikoa ya kanda ya kati.
Amesema, kanda hiyo ilijulikana sana kuwa ngome ya CCM, lakini amefanikiwa kuchaguliwa na wananchi ili awatumikie.
No comments:
Post a Comment