Monday, February 6, 2012

HABARI KUTOKA MUSOMA


MUSOMA

MENEJA UTUMISHI WA KAMPUNI YA UCHIMBAJI VISIMA YA MASWI DRILLING CO LTD MAUNGO MICHAEL AMESEMA KUWA UMEFIKA WAKATI AMABAPO SERIKALI INATAKIWA KUANGALIA WACHIMBAJI WASIO NA SIFA KUTOPEWA KAZI.
AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI MJINI MUSOMA MENEJA HUYO AMESEMA KUWA KUMEKUWEPO NA BAADHI YA KAMPUNI AMBAZO HAZINA SIFA WALA VIFAA LAKINI ZIMEKUWA ZIKIPATA NAFASI KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA UMMA.
 BW. MAUNGO AMESEMA KUWA NI VYEMA KAMPUNI KAMA HIZO ZIKAANGALIA KUWEKA MSILAHI YA UMMA MBELE NA SI MASILAHI YAO KWANI KWA KUFANYA HIVYO NI KUHARIBU FEDHA ZA UMMA.
AMESEMA KWA MWAKA WA 2010 KAMPUNI YAKE YA MASWI DRILLING CO.LTD IMEFANIKIWA KUCHIMBA VISIMA  102 BAADHI YA MAENEO HAPA NCHINI AMBAPO KATI YA HIVYO NI VIJIJI  15 PEKEE AMBAVYO HAVIKUPATA MAJI.
AIDHA AMESEMA KUWA ANASHANGAZWA NA HALI YA WATU KUCHANGANYA TAALUMA NA SIASA KITU AMBACHO AMESEMA KINAWEZA KUSABABISHA KUPELEKEA  UTENDAJI KAZI WA KZI ZA UMMA KUWA MBOVU.
AIDHA AMESHTUMU BAADHI YA MAKANDARASI MKOANI MARA KUENDELEZA MBINU CHAFU ZA KIBIASHARA AMBAPO AMESEMA KUWA KAMWE MBINU HIZO HAZITAJENGA BALI ZITABOMOA
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

WITO UMETOLEWA KWA WAFANYA BIASHARA MKOANI MARA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZINAWEKWA NA SERIKALI KUTOKANA NA KUPEWA MUDA MREFU WA KUHAMA KATIKA MAENEO YA BARABARA AMBAYO HAYATAKIWA KUTUMIWA KWA KAZI YOYOTE.

AKIONGEA NA VICTORIA FM OFISINI KWAKE LEO ASUBUHI KAIMU AFISA BIASHARA MANISPAA YA MUSOMA GODFREY MACHUMU AMESEMA KUWA SERIKALI IMETOA MAENEO YA WAFANYABIASHARA NA KUWAPA MUDA WA KUHAMA KATIKA MAENEO YALIYOTENGWA NA SERIKALI

AMESEMA KUWA LICHA YA KUTOLEWA TAARIFA KWA WAFANYABIASHARA HAO KUHAMA KATIKA MAENEO HAYO LAKINI WAMEKAIDI AGIZO HILO MPAKA MAMLAKA YA BARABARA MKOANI MARA TANROADS ILIPO CHUKUA HATUA YA KUBOMOA VIBANDA HIVYO KATIKA ENEO LA BARABARA YA MAJITA.

AMEONGEZA KUWA WAFANYABIASHARA WADOGO TAYARI WAMEPEWA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO LA KAMNYONGE NA ENEO LA MTAKUJA WAMEPEWA WAFANYABIASHARA WAKUBWA WENYE MADUKA AMBAPO WAMEELEZWA WATAJENGA MADUKA KWA GHARAMA ZAO AMBAPO HAWATATOZWA KODI.

AIDHA KAIMU AFISA HUYO WA BIASHARA MANISPAA YA MUSOMA AMEONGEZA KUWA LENGO LA SERIKALI NI KUTOA MAENEO BORA AMBAYO WAFANYABIASHARA WATAFANYA BIASHARA ZAO PASIPOKUSUMBULIWA.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

WANANCHI MKOA WA MARA WAMETAKIWA KUACHA TABIA ZA KUKAA VIJIWENI NA KUITUHUMU SERIKALI KWA MAMBO YASIYO NA UKWELI NA KUZINGATIA SHERIA PAMOJA TARATIBU ZINAZOWEKWA NA SERIKALI

HAYO YAMESEMWA NA MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA MUSOMA ALEX KISURURA WAKATI AKIZUNGUMZA NA VICTORIA FM KATIKA OFISI YAKE LEO HII

AMESEMA KUWA SERIKALI HAINA NJIA NYINGINE YA KUWASAIDIA WAHANGA WA BOMOABOMOA KATIKA ENEO LA BARABARA YA MAJITA KWANI TAARIFA IMETOLEWA KWA MUDA MREFU NA KUWALIPA FIDIA ZINAZOSTAHIKI

AIDHA AMEONGEZA KUWA SERIKALI IMETENGA VIWANJA 1384 NA KUUZA KWA GHARAMA NAFUU KWA WATU WOTE VIWANJA HIVYO VIKO KATIKA MAENEO MBALIMBALI MANISPAA YA MUSOMA, AMBAPO AMEYATAJA MAENEO HAYO KUWA NI SONGAMBELE, BWERI, NYABISALE SEKONDARI, NYAMIONGO,KIYARA,BUHARE NA BUKANGA

AMEBAINISHA KUWA CHANGAMOTO MBALI MBALI ANAZOKUTANA NAZO IKIWA NI KUTENGENEZA MIUNDO MBINU,SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI,SEKTA YA AFYA NA KUONGEZA KUWA MAHITAJI YA WATU NI MENGI KUZIDI UWEZO WALIONAO MANISPAA.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

BUNDA


VIJANA WILAYANI BUNDA MKOANI MARA WAMEMLALAMIKIA MBUNGE WA JIMBO HILO STEVEN WASIRA KWA KUTOA AHADI ZA KUWAWEZESHA  VIJANA HAO LAKINI MPAKA SASA AMESHINDWA KUTIMIZA AHADI  HIYO NA KUPELEKEA VIJANA HAO KUJIUNGA KATIKA MAKUNDI MABAYA

WAMESEMA NI VYEMA SERIKALI IKATEKELEZA AHADI INAZOTOA IKIWA NI NJIA YA KUWASAIDIA VIJANA HAO KUPAMBANA NA MAISHA, KATIKA AHADI AMABZO MBUGE HUYO ALIAHIDI NI PAMOJA NA KUWATAFUTIA NAFASI ZA KAZI SEHEMU MBALIMBALI NA WENGINE KUWAPELEKA JESHINI LAKINI AHADI HIZO HAJAZITEKELEZA MPAKA SASA

PAMOJA NA HAYO  MWENYEKITI WA KATA YA BUNDA MJINI ERNEST NKONOKI   AMEWATAKA VIJANA HAO KUWA NA UVUMILIVU MPAKA HAPO MBUNGE  HUYO  ATAKAPO TOKA BUNGENI MJINI DODOMA  KUSHUGHULIKIA HILO.

HATA HIVYO MWENYEKITI HUYO AMETOA WITO KWA VIJANA HAO KUTOBWETEKA NA KUSUBIRI KUWEZESHWA WAO WENYEWE WANAWEZA KUJIAJIRI NA SIO KUMTEGEA MTU  KWANI WANATAKIWA WAJIFUNZE KUJITEGEMEA      
 
SANJARI NA HAYO WAKAZI  WILAN BUNDA WAMELALAMIKIA JESHI LA POLICE   AMBAPO   WAMESEMA KUWA WAMESHINDWA KUTEKELEZA MA JUKUMU YAO  KAMA WALIVYO KULA KIAPO KABLA YA KUINGIA KAZINI BADALA YAKE WAO KUANZA KUSHILIKIANA NA WAHALIFU MJIN BUNDA.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment