MUSOMA
CHAMA CHA MAPINDUZI CCM TAIFA,KIMESEMA KIMERIDHISHWA KWA KIASI KIKUBWA NA HALI YA AMANI AMBAYO IMEANZA KUPATIKANA MKOANI MARA,JAMBO AMBALO SASA LIMEANZA KUTIA MATUMAINI KWA MKOA HUO KUVUTIA KWA SHUGHULI ZA UWEKEZAJI.
KWA SABABU HIYO CCM IMESEMA KUREJEA KWA AMANI YA KUDUMU MKOANI MARA KUTAWEZESHA KUHARAKISHA MAENDELEO YA WANANCHI NA KUCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI KUTOKANA NA KURUHUSU WATU KUJISHUGHULISHA.
KAULI HIYO IMETOLEWA MJINI MUSOMA NA KATIBU WA SIASA,ITIKADI NA UENEZI WA CCM TAIFA BW NAPE NNAUYE,WAKATI AKIZUNGUMZA NA UONGOZI WA MKOA WA MARA,AMBAPO AMESEMA CCM IMERIDHISHWA NA JINSI SERIKALI YAKE YA MKOA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VINAVYOSIMAMIA UREJESHAJI WA AMANI MKOANI MARA.
HATA HIVYO AMESEMA SERIKALI YA MKOA INAPASWA KUHIMIZA VYOMBO VYAKE VYA ULINZI NA USALAMA KUWEKA MIKAKATI THABITI ITAKAYO WEZESHA AMANI KUTOTETEREKA TENA.
MKOA WA MARA HASA KATIKA WILAYA YA TARIME NA RORYA,KWA ZAIDI YA MIAKA 20 UMEKUWA NA MATUKIO YA MAPIGANO YA KOO,WIZI WA MIFUGO,MAUJI YA MARA KWA MARA HASA YA KULIPIZANA VISASI HATUA AMBAYO ILICHANGIA KUKOSEKANA KWA AMANI YA KUDUMU NA KUDHOROTESHA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO YA WANANCHI.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
WITO UMETOLEWA KWA WAZAZI NA WALEZI MKOANI MARA KUWALINDA NA KUWATUNZA WATOTO DHIDI YA TABIA HATARISHI ZINAZOWAKABILI NA KUSABABISHA ONGEZEKO LA WATOTO WA MITAANI.
KAULI HIYO IMETOLEWA JANA NA SAJENTI ZUHURA NA SAJENTI ANOLD AMBAPO WAMEBAINISHA KUWA BAADHI YA MAMBO YANAYOFANYIKA KWA WATOTO SI MASLAHI BORA YA MTOTO NA KUWA HATUA ZA JUMLA ZA KUMLINDA MTOTO ZINAHITAJIKA
SAJENTI ANORLD AMEBAINISHA KUWA MASLAHI BORA KWA MTOTO YATAKUA MATENDO YA MSINGI YANAYOMHUSU MTOTO IKIWA NI PAMOJA NA HAKI YA KUISHI,HAKI YA UTAMBULISHO,HAKI YA ULINZI NA USALAMA NA HAKI YA KUSHIRIKI KWA KUTOA MAWAZO YAO NA KUSIKILIZWA MAAMUZI YANAYOHUSU MASLAHI YAO.
SAJENTI ZUHURA AMEONGEZA KUWA KUNA HATUA ZA JUMLA ZA KUMLINDA MTOTO AMBAZO NI KUMLINDA KUTOKANA NA HATARI YA MAENEO, HATARI YA TABIA, HATARI YA KUTUMIKISHWA,KUTELEKEZWA,NA UNYANYASAJI.
AIDHA AMESEMA KULINGANA NA MAKOSA HAYO SHERIA INASEMA ADHABU YAKE NI FAINI ISIYOZIDI SHILINGI LAKI TANO AU KIFUNGO KISICHOZIDI MIEZI SITA AU VYOTE VIWILI.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment