Monday, January 9, 2012

RAIS WA GUINEA BISSAU AFARIKI DUNIA

Rais wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha, amefariki dunia katika hospitali moja mjini Paris, nchini Ufaransa, alipokuwa akipokea matibabu.

Afisa mmoja  wa serikali ya Ufaransa leo ametangaza kifo cha kiongozi huyo wa taifa hilo la magharibi mwa Afrika ambalo limekumbwa na misukosuko.

Sanha ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 64, alilazawa katika hospitali ya kijeshi ya Val de Grace muda mfupi kabla ya sikukuu ya krismasi. 


Ugonjwa uliosababisha kifo chake haujatangazwa kwa umma, lakini afisa huyo wa Ufaransa amesema amekuwa katika hali mahututi kwa muda sasa.

 Tangu kuingia madarakani mwaka 2009, Sanha amekuwa akisumbuliwa na afya mbaya, na aliondoka mwezi Novemba mwaka jana kutafuta matibabu ng' ambo na kuzua wasiwasi wa serikali yake kupinduliwa na jeshi katika nchi ambayo imeshuhudia mapinduzi kadhaa.

No comments:

Post a Comment