MUSOMA
MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA MJINI VINCENTI NYERERE AMESEMA KUWA HAKUNA MWANANCHI YOYOTE ATAKAYECHANGIA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA KWA SASA KWA KUWA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA IMETENGA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 75 KWA AJILI YA KAZI HIYO.
HAYO AMEYASEMA JANA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MKENDO ALIPOKUWA AKIWAELEZEA WANANCHI YALE ALIYOYAFANYA KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA KWA MWAKA MMOJA KATIKA JIMBO LA MUSOMA MJINI.
MH NYERERE AMEDAI KUWA YALE YANAYOELEZWA NA BAADHI YA WATU KUWA WAMEGOMESHA UCHANGIAJI WA UJENZI WA MADARASA WANAPOTEZA MUDA KWA KUWA HIYO ILIKUWA NI MOJA YA AHADI ZILIZOTOLEWA NA CHAMA HICHO KILICHO NA DHAMANA YA UONGOZI KATIKA KIPINDI CHA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2010.
AMESEMA KUWA WANAFUNZI WOTE WALIOFAULU KUINGIA KIDATO CHA KWANZA WATAKWENDA SHULENI KWA KUWA KWA SASA KUNA KASI KUBWA YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA ILI KUKABILIANA NA UPUNGUFU ULIOJITOKEZA.
MBUNGE HUYO WA JIMBO LA MUSOMA MJINI AMEONGEZA KUWA LICHA YA KUENDELEA KWA UJENZI WA VYUMBA HIVYO VYA MADARASA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA PIA AMETENGA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 22 NA LAKI NNE KWA AJILI YA UTENGENEZAJI WA MADAWATI 305 KWA AJILI YA KUKABILIANA UHABA WA MADAWATI.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
HALI YA UHALIFU IMEPUNGUA MKOANI MARA KATIKA KIPINDI CHA JULAI 2010 HADI JUNI 2011.
KATIKA TAARIFA ILIYOSOMWA KWENYE KIKAO CHA WAJUMBE WA HALMSHAURI KUU YA CCM MKOA WA MARA HIVI KARIBUNI IMESEMA KUWA KUMEKUWEPO NA MATUKIO MACHACHE YALIYOJITOKEZA KAMA WIZI WA MIFUGO, MADAWA YA KULEVYA NA UVAMIZI WA MGODI WA NORTH MARA.
MATUKIO MENGINE YALIYOELEZWA KATIKA KIKAO HICHO NI PAMOJA NA MAUAJI YATOKANAYO NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MIKONONI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WANAOTUHUMIWA KWA UHALIFU.
AIDHA UVAMIZI WA VITUO VYA POLISI NI MOJA YA MATUKIO AMBAYO YAMETOKEA KATIKA KIPINDI HICHO WILAYANI SERENGETI NA WILAYA YA BUNDA MKOANI MARA.
MBALI NA HIVYO HALI YA WAFANYABIASHARA KUSAFIRISHA SUKARI NA MAHINDI NJE YA NCHI SERIKALI ILICHUKUA HATUA MADHUBUTI IKIWA NI NJIA YA KULINDA UTOROSHAJI HUO.
KATIKA KUKABILIANA NA HALI HIYO TAARIFA HIYO IMEELEZA KUWA SERIKALI IMECHUKUA HATUA YA KUTOA ELIMU YA ULINZI SHIRIKISHI HUKU JITIHADA ZA KUWAHAMASISHA WAFUGAJI KUFANYA DORIA ZA ULINZI WA MIFUGO KUSAIDIANA NA JESHI LA POLISI.
TAARIFA HIYO IMEELEZA KUWA HALI YA USALAMA KWASASA IMEIMARIKA KUTOKANA NA OPERESHENI ILINAYOFANYWA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA PAMOJA NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
WANANCHI MKOANI MARA WAMESEMA KUWA WAHUDUMU KATIKA SEKTA YA AFYA WANAPASWA KUFUATA MAADILI YA TAALUMA HIYO HUKU WAKIZINGATIA PIA LUGHA WAZITOAZO WAKATI WAKIWA KATIKA KUTIMIZA MAJUKUMU YAO.
WAKIONGEA LEO KATIKA KIPINDI CHA ASUBUHI CHA BIG BREAKFAST WANANCHI HAO KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI MKOANI MARA WAMESEMA VITENDO VINAVYOFANYWA NA WAUGUZI NA MADAKTARI SI VYA KIUNGWA KWANI KWA KUFANYA HIVYO WANAJENGA CHUKI KATIKA JAMII.
WAMESEMA NI MTUMISHI WA AFYA AMBAYE ANAONA HAWEZI KUTO HUDUMA NZURI KWA MGONJWA NI VYEMA AKAJIONDOA KATIKA TAALUMA HIYO INAYOTAKIWA KUONYESHA UPENDO KWA MGONJWA
KAULI HIZO ZA WANANCHI ZIMEFUATIA BAADA YA VICTORIA FM JANA KUSHUHUDIA HAKUNA MADAKTARI KATIKA HOSPITAL YA MKOA WA MARA, WODI ZIKIWA CHAFU HUKU BAADHI YA WAUGUZI WAKIWAFUNGIA WAGONJWA WODINI.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment