BUNDA
KITUO CHA KUWAJENGEA WANANCHI UWEZO KUHUSU HAKI ZA BINADAMU (CARH) CHA MJINI BUNDA KIMELAANI KITENDO CHA WANANCHI WA KIJIJI CHA MWIBAGI KATA YA KYANYARI KATIKA WILAYA YA MUSOMA VIJIJNI CHA KUJICHUKULIA SHERIA MIKONONI NA KUWACHOMEA WENZAO NYUMBA NA MALI ZAO WAKIWATUHUMU WACHAWI NA KUITAKA SERIKALI IDHIBITI HALI HIYO ISIZIDI KUTOKEA NCHINI.
TUKIO HILO LIMETOKEA SIKU MBILI MFULULIZO KATI YA JANUARI 5 NA 6 MWAKA HUU WANANCHI WA KIJIJI HICHO CHA MWIBAGI WALIZICHOMEA NYUMBA NA MALI ZAO MBALIMBALI IKIWAMO MIFUGO NA VYAKULA KAYA 16 ZA KIJIJI HICHO WAKIZITUHUMU KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA KISHIRIKINA.
KATIKA TUKIO HILO LILISABABISHA KUVURUGA AMANI NA USALAMA WA KIJIJI HICHO HUKU WAKIENDELEA KUWASAKA WAHUSIKA ILI WAWAUWE.
HATA HIVYO BAADA YA SERIKALI NGAZI YA WILAYA KUPATA TAARIFA ZA UWEPO WA TUKIO HILO ILIINGILIA KATI KWA KUTUMA JESHI LA POLISI KIJIJINI HAPO KUZIMA TUKIO HUKU.
MKUU WA WILAYA YA MUSOMA KAPTENI MSTAAFU GEOFFREY NGATUNI KUPITIA MKUTANO WA HADHARA ALIWATAKA WAKAZI HAO KUTOJICHUKULIA SHERIA MIKONONI NA BADALA TAKE WAVIACHIE VYOMBO VYA DOLA VIFANYE KAZI YAKE.
KWA MUJIBU WA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ILIYOTOLEWA NA KITUO HICHO JANA KITENDO CHA WANANCHI HAO KUWACHOMEA WENZAO NYUMBA NA MALI ZAO VIKIWAMO VYAKULA NI MOJA YA VITENDO VYA UKIUKAJI WA HAKI ZA BINADAMU VINAVYOTAKIWA KUDHIBITIWA KIKAMILIFU NA SERIKALI ILI VISIHATARISHE HALI YA AMANI NA UTULIVU NCHINI.
KUPITIA TAMKO HILO LA KITUO HICHO IMESEMA KUWA KAMA KULIKUWA NA TUHUMA ZOZOTE ZA KISHIRIKINA AU ZA UJAMBAZI DHIDI YA WATU HAO WANANCHI HAO WANGETUMIA TARATIBU ZA KISHERIA AMBAZO NI KUWAKAMATA NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA DOLA BADALA YA KUWAFANYIA WENZAO VITENDO HIVYO VYA KIKATILI VILIVYO KINYUME NA HAKI ZA BINADAMU.
HIVYO KITUO HICHO MBALI NA KUTOA RAI KWA WANANCHI KUACHANA NA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MIKONONI PIA KIMETUMIA FURSA HIYO KUIOMBA SERIKALI NA VYOMBO VYAKE VYA DOLA KUWASAKA NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA WALE WOTE WALIOHUSIKA KATIKA VITENDO HIVYO HUKU IKIWASAIDIA WAHANGA WA TUKIO HILO KUPATA HAKI ZAO MSINGI IKIWAMO HIFADHI YA MAISHA.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
MUSOMA
WANANCHI MKOANI MARA WAMELALAMIKIA HATUA YA EWURA KUTANGAZA BEI MPAYA YA UMEME HII LEO KWANI KWA KUFANYA HIVYO WAMESEMA KUNASABABISHA ONGEZEKO LA GHARAMA ZA MAISHA KWA MTANZANIA.
WAKICHANGIA LEO ASUBUHI KATIKA KIPINDI CHA BIG BREAKFAST WANANCHI HAO KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI MKOANI MARA WAMESEMA KUWA KUPANDISHA KWA GHARAMA HIZO NI KUWAKANDAMIZA WATANZANI.
WAMESEMA BADO SHIRIKA LA UMEME TANZANIA LIMESHINDWA KUPELEKA UMEME VIJINI LAKINI WAMEKUWA MAKINI KATIKA KUANGALIA JINSI GANI YA KUMKANDAMIZA WANANCHI.
WANANCHI HAO WAMESEMA KUWA UMEFIKA WAKATI AMBAPO TANZANIA INAHITAJI KUWA NA MASHIRIKA MBALIMBALI YA UMEME KWANI KWA KUFANYA HIVYO KUTASAIDIA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UMEME.
NOVEMBA 9 MWAKA JANA, EWURA ILIPOKEA OMBI LA DHARURA KUTOKA TANESCO LA KUIDHINISHIWA ONGEZEKO LA BEI ZA HUDUMA YA UMEME KWA WASTANI WA ASILIMIA 155 YA BEI YA SASA KWA MADAI KUWA WANAINGIA GHARAMA KUBWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUZALISHA UMEME WA DHARURA.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
RORYA
ZAIDI YA WANAFUNZI 520 AMBAO WAMECHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA HUU KATIKA WILAYA YA RORYA MKOANI MARA,WATALAZIMIKA KUSOMEA CHINI YA MITI KUTOKANA NA UHABA MKUBWA WA VYUMBA VYA MADARA UNAOZIKABILI SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI HUMO.
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA BW COSMAS NGANGAJI,AMEYASEMA HAYO KWA NYAKATI TOFAUTI KATIKA KATA ZA NYAMAGALO NA MILALE, WAKATI WA KUHAMASISHA UJENZI WA VYUMBA HIVYO VYA MADARASA.
AMESEMA PAMOJA SERIKALI KUPITIA HALMASHAURI KUTOA SHILINGI MILIONI 15 KWA KILA SHULE KWAAJILI YA KUSADIA UJENZI WA VYUMBA HIVYO LAKINI NI WAJIBU WA WAZAZI KUCHANGIA NGUVU ZAO KATIKA KUHAKIKISHA WATOTO HAO WANAPATA MAHALA PA KUSOMEA.
KWA UPANDE WAKE MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA RYAGORO BI MUGURE MIGO AMESEMA SHULE YAKE IMEPANGIWA KUCHUKUA WANAFUNZI 147, LAKINI VYUMBA VILIVYOPO VINAUWEZO WA KUCHUKUA WANAFUNZI 90.
KATIKA HILO AMESEMA WANAFUNZI 67 WATAKOSA NAFASI HUKU MKANDARASI AMBAYE AMEJITOLEA KUSADIA UJENZI HUO BW MOSES SIGORI AKIWAOMBA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO ILI KUHAKIKISHA KAZI HIYO INAKAMILIKA KWA WAKATI.
AKIZUNGUMZA KATIKA MIKUTANO HIYO, MBUNGE WA JIMBO LA RORYA MH LAMECK AIRO,PAMOJA NA KUHAMASISHA UJENZI HUO,AMEWATAKA WANANCHI HAO KUPAMBANA NA VITENDO VYA UHALIFU HASA WIZI WA MIFUGO IKIWA NI PAMOJA NA KUWATENGA WATU WANAJIHUSISHA NA VITENDO HIVYO NDANI YA JAMII.
KATIKA ZIARA HIYO MBUNGE HUYO WA JIMBO LA RORYA,AMETOA AHADI YA KUWASOMESHA WANAFUNZI WATANO KWA KILA SHULE YA SEKONDARI WILAYANI RORYA AMBAO NI YATIMA NA WALE WANAISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU PAMOJA MADAWATI 70 AMBAYO YATATUMIWA NA WANAFUNZI HAO KATIKA SHULE 25 ZA SEKONDARI WILAYANI RORYA.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment