Serikali ya Kenya imetenga dola milioni 22.2 kwa ajili ya mpango wa chakula shuleni kuhakikisha kuwa wanafunzi katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame wanapata huduma hiyo.
Hayo yamesemwa na rais Mwai Kibaki wa Kenya jijini Nairobi kwenye tamasha la muziki la kitaifa la mwaka huu. Amesema kuwa mpango wa kutoa chakula shuleni katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame utaendelea hata wakati wa mapumziko.
Watu takriban laki 7 katika wilaya za Turkana, Marsabit, Isiolo, Mandera, Wajir na Garissa kaskazini mwa Kenya wanahesabiwa kuwa na uhaba wa chakula.
No comments:
Post a Comment