Wednesday, August 10, 2011

KATIBU WA CHAMA CHA MPIRA ALIYECHAGULIWA APINGWA,WAHOJI ELIMU YAKE,

Serengeti

UCHAGUZI wa chama cha miguu wilaya ya Serengeti umepingwa kutokana na katibu aliyechaguliwa Francis Magati kubainika kutowasilisha vyeti vya shule aliyosoma kama kanuni za TFF zinavyoelekeza.

Julai 29 mwaka huu uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wahalmashauri ya wilaya ambapo Magati alishinda kwa kura 16 dhidi ya 9 za Barnabas Makaranga aliyekuwa akigombea nafasi hiyo.

Kwa mjibu wa barua ya kusudio la kukata rufaa ya agosti 2,mwaka huu inabainisha kuwa kanuni zilikiukwa kwa kumpitisha kugombea bila kuonyesha vyeti vya shule aliyosoma ,badala yake akawasilisha barua ya polisi kuwa alipotelewa na vyeti.

Barua ya rufaa iliyowasilishwa kwa mwenyekiti wa uchaguzi mkoa wa Mara inabainisha kuwa kanuni d sura ya 9 no.2 kwa kumpitisha kinyume Magati wakati hana sifa za kugombea nafasi hiyo ,kisha kutangazwa kuwa katibuwa chama cha mpira wa miguu wilaya.

Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mara katika barua yake
yenye kumb.Na.FAM/MR/UCH.04 ya agosti 5,2011 inakiri kupokea barua ya
rufaa dhidi ya katibu .

Barua hiyo iliyosainiwa na katibu wa chama hicho Magoti inabainishakuwa kamati ya uchaguzi itakutana agosti 11 saa 4 asubuhi ukumbi wa uwanja wa ndege Musoma ,huku Magati akitakiwa kuwasilisha vielelezo vya vyeti vyake halisi vya alikosoma.

Mchakato wa kukata rufaa ulibainika kuungwa mkono na wadau mbalimbali
wa michezo ambao walilazimika kuchangia tsh,200,000= kama gharama za
rufaa.

Katika uchaguzi huo diwani Donald Ntogocho alichaguliwa kuwamwenyekiti wa chama hicho na kuahidi mambo makubwa.

Hata hivyo kampeini zilijikita kikabila zaidi na kisiasa hali ambayoililalamikiwa na wadau wengi wa michezo wilayani hapo.

No comments:

Post a Comment