Saturday, July 30, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA JESHI LA POLISI

2. Mnamo tarehe 22/7/2011 Inspekta Jenerali wa Polisi Said Alli Mwema alitoa wito kwa wananchi wote kupitia vyombo vya habari kuwa, katika utekelezaji wa kampeni ya kutii sheria bila kushurutishwa wale wote wanaomiliki silaha isivyohalali wazisalimishe kwa hiari na zinazomilikiwa kihalali zihakikiwe upya. Na zoezi hili ni kwa muda wa miezi mitatu (3) kuanzia tarehe 1 Agosti hadi Octoba 31, 2011. Katika kipindi hicho hakutakuwa na hatua zozote za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya mtu atakayesalimisha/kuhakiki silaha kwa hiari yake.

3. Tunawashukuru wananchi ambao wameanza kuitikia wito huo kwa kuanza kusalimisha silaha zao kwa hiari. Pamoja na hayo, inaonekana bado kuna makundi ya watu/watu ambao bado wanaendelea kumiliki na kufanyia uhalifu silaha wanazozimiliki isivyo halali. 

4. Mfano wa matukio hayo ni kama ifuatavyo, mnamo tarehe 28/7/2011 majira ya saa 7 usiku katika Mkoa wa Kagera wilaya ya Biharamuro, wananchi wema walitoa taarifa polisi kuwa, kuna majambazi yapatayo 6 katika eneo la pori lililopo kati bwanga na Bihalamuro wamejipanga kuteka magari ya abiria/ mizigo yanayopita katika eneo hilo, baada ya polisi kupata taarifa hizo, walienda katika eneo hilo na ghafla majambazi hayo yalianza kuwafyatulia risasi. Katika kurushiana risasi Polisi walifanikiwa kuyaua majambazi yote sita (6) na kufanikiwa kupata silaha 2 aina ya SMG na risasi 180.

5. Aidha, katika tukio jingine la kusikitisha mnamo tarehe 27/7/2011 majira ya usiku huko katika kijiji cha Genkuru Tarime Rorya askari Polisi No. F. 4268 D/C Pendo aliuawa kwa kupigwa risasi shingoni na jambazi aitwae Bhoke Mohere waliyekuwa wameenda kumkamata nyumbani kwake kwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha na kumiliki silaha isivyo halali. Baada ya mauaji hayo jambazi hilo lilifanikiwa kutoroka.

6. Hali hii, inadhihirisha wazi ni jinsi gani askari polisi wanafanya kazi katika mazingira hatarishi, pamoja na kwamba wanakuwa wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata matakwa ya sheria, lakini kuna mahali wanakutana na mazingira ya watu wabaya wanaokaidi kutii sheria, hali inayopelekea askari wenyewe kuuawa ama kujeruhiwa. Na hii ina maana kwamba nguvu anayoitumia mhalifu katika kupambana na askari ndiyo inayomlazimu askari Polisi kuona atumie nguvu kiasi gani ili aweze kumdhibiti mhalifu huyo.

8. Wito wangu kwa jamii, wakati zoezi hili linaendelea nawaomba wananchi wote waendelee kutoa taarifa za watu wanaowafahamu ambao wanamiliki silaha isivyohalali ili kusaidia kuwabaini endapo watakaidi agizo la kusalimisha silaha hizo kwa hiyari.
 
Imeandaliwa na
Advera Senso- ASP
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania.

No comments:

Post a Comment