Friday, July 29, 2011

MUBARAK KUPANDA KIZIMBANI WIKI IJAYO HUKO CAIRO

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak pamoja na matatizo ya afya anategemewa kufikishwa kizimbani wiki ijayo.
Rais wa zamani Misri Honi Mubarak.
Picha Rais wa zamani Misri Honi Mubarak. 
Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak atakabiliwa na kesi wiki ijayo mjini Cairo.

Maswali juu ya afya ya Bw. Mubarak yamepelekea uvumi  kuwa kesi yake inaweza kuahirishwa au kufanyika katika eneo la mapumziko la Shamelsheikh ambako anatibiwa.
Lakini vyombo vya habari vilimkariri naibu  waziri wa sheria akisema kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa Agosti 3 na kufanyika huko Convention Centre mjini Cairo.

Bw. Mubarak anashitakiwa kwa rushwa na kuamuru  mauaji ya waandamanaji. Karibu watu 900 waliuwawa wakati wa mapinduzi ya siku 18 yaliyomwondoa madarakani mwezi February.

No comments:

Post a Comment