Tuesday, July 19, 2011

MWANAMKE TARIME AKATWA KIGANJA NA MMEWE

Na  Waitara Meng’anyi, Tarime.
 Mwanamke mmoja mkazi wa  Nyabiroga Songa Bunchari  Wilayani Tarime Agnes Chacha (25)  amefyekwa kiganja chake cha mkono na magoti yote mawili na mume wake Chacha Hamis jana usiku  na amelazwa katika wod 6 hosptali ya wilaya akipata matibau.
Akizungumza kwa uchungu  na kulia kwa  maumivu makali  ya majeraha  wodini hapo Agnes alismakuwa jana majira ya saa mbili mume wake alimkata kigaja chake na kutoroka kusiko julikana.
“ Baada ya kunikata alikimbia akiniacha  nimezimia nilipoamka sikumkuta” alieleza Agines akiwa kitandani

Alisema kuwa jana alifika nyumbani saa mbili usiku akitoka dukani kwao na kuwa kulikuwa na wateja wengi kwa kuwa ilikuwa siku ya soko  ambapo mara nyingi huwa wanachelewa wakati mwingine wakiwa na mume wake.
“ Haikuwa mara yangu ya kwanza kuingia nyumbani muda kama huo ila sijui kwa nini alifanya hivi?” alieleza kwa masikitiko.
Akiendelea kuzungumza kwa  alisema kuwa baada ya kufika nyumbani aliwaagiza watoto wake kumfuatia unga wa muhogo kwa wifi yake ambapo watoto walimwambia kwamba wanaogopa kwani ulikuwa usiku hivyo akalazimika kubandika maji jikoni na kwenda mwenyewe.
Alisema baada ya kutoka kwa wifi yake akiwa na unga wake alimkuta mume wake akiwa amekaa nje ameshika panga lake, alimwuliza sababu za yeye kufikia nje akiwa na panga na  mumewe kusema kumuuliza alikokuwa.
“ Mimi nina mimba ya mwezi mmoja imenisababishia kuuchukia ugali wa mahindi ndio maana nilifata mwenyewe licha ya kwamba ulikuwa usiku lakini mume wangu hakutaka kunisikiliza japo nilikuwa na unga akaanza kunilazimisha niseme nilikuwa wapi na nilikuwa na nani” alisema.
Akiendelea kuzungumza alisema kuwa baada ya kuona mumewe anamlazimisha kusema aliekuwa nae ili amsamehe aliamua kusema alikuwa na Muhiri kijana ambaye mume wake huyo amekuwa akimlazimisha kuwa ni mpenzi wake baada ya kuwa amepata maneno kwa watu.
Alifafanua kuwa mume wake aliwahi kufungwa kipindi cha vita ya koo aliporudi uraiani watu walimwambia kwamba mke wake Bi Agnes alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Muriri hivyo mume wake hivyo anahisi aliweka kinyongo tangu kipindi hicho ingawa anadai wanaishi vizuri.
 Agnes alisema “baada ya watoto wangu kuona nimekatwa  kiganja na kuruka mbali walipiga yowe hivyo watu wakakusanyika baada ya kupata fahamu nilimkuta shemeji yangu,wifi yangu pamoja na mke mwenzangu ambao  wakifanya jitihada za kupata gari  kunipeleka hosptali”
Licha ya Bi.Agnes kufanyiwa ulemavu wa maisha alisema akipona atarudi kwa mume wake kwa sababu  watoto wake watapata shida na  hawezi kupokelewa na mtu mwingine akiwa na mkono mmoja ikiwa ni pamoja na kukosa ajira yoyote akiwa ulemavu.
Muuguzi wa zamu ambaye hakupenda jina lake kutajwa alisema  waliokuwepo katika zamu usiku waligoma  kumtibu wakitaka barua toka polisi hadi hivi  leo asubuhi baada ya kuona wauguzi wamembana sana kusema ukweli alisema polisi walifika wodini hapo  kuchukuwa maelezo yake.
“ wifi yake alikuwa hapa akiwa  anaficha siri ila  tukajua kuwa ni mume wake amemkata na kweli ni mume  yaani matukio kama haya ni mengi hapa hata wengine walikuwa hapa ” alisema
Amewataja watu hao kuwa ni Nyangi Wansama Ryoba mkazi wa Nyamongo (31) aliyekatwa mgongo na mume wake ambaye ameruhusiwa kuondoka leo na mwingine ni Deborah Lucas Jockson(38) mkazi wa Buhemba  nje kidogo na mji wa Tarime ambaye amepigwa na kuumizwa vibaya maeneo ya nyonga na mbavuni.
Wagonjwa waliolazwa wodini humo wamesema mama huyo ameamua kutoroka kwenda kwa dada yake kabla yakuruhusiwa baada ya mume wake kufika hosptalini hapo leo asubuhi na kumtishia kuwa siku akitoka hosptalini asiende kwake atamwua.
“ Ametwambia kuwa ataenda kwa dada yake nahisi ametoroka kwenda huko manake mume wake amesema atamwua hata huyo mwuguzi atakwambia hayupo” walisema.
Hata hivyo Kamanda wa jeshi la polisi Deusdedit Katto  hakuweza kupatikana kwa haraka kuzungumzia jambo hili  baada ya kupigiwa simu yake na kutopatikana.
Mwisho

1 comment:

  1. Tunapaswa kuendelea kuelimisha jamii yetu ili tutokomeshe matukio ya kinyama ya namna hii!

    Aidha hakuna uhalali wa kumnyima mtu huduma za afya eti mpaka aonyeshe barua ya polisi. Huduma kwanza (tuokoe maisha ya watu) mengine yafuate!

    ReplyDelete