WATU wasiojulikana wameingilia mawasiliano ya mtandao ya Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kuanza kuutumia kwa masuala hayo ikiwa ni pamoja na kufanya vitendo vya kitapeli kwa kutumia mawasiliano (e-mail).
Matapeli hao wa mtandao walifanikiwa kuingia katika mawasiliano hayo ya siri ya katibu huyo, jana ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Wahariri nchini ambao ulijadili masuala nyeti ya kitaifa ikiwemo tasnia ya habari na maslahi ya taifa.
Aidha matapeli hao kwa kutumia e-mail ya Katibu Mkuu huyo, Nevilli Meena ambaye pia ni Mhariri wa Gazeti la Jumamosi la Mwananchi, wamekuwa wakiwatumia baadhi ya marafiki wa karibu wa Meena kufanya utapeli huku wakionesha kutaka kutumiwa fedha kiulaghai.
Akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu, Mhariri Mkuu huyo amethibitisha mtandao wake (e-mail) kuingiliwa na matapeli wa mtandao tangu jana na wamekuwa wakituma taarifa kwa baadhi ya marafiki zake kuomba watumiwe fedha.
“Ni kweli e-mail yangu imeingiliwa na baadhi ya watu na wamekuwa wakituma taarifa za uongo kwenda kwa rafiki zangu ambao ninawasiliana nao mara kwa mara…nimepokea simu nyingi watu wakidhani mimi namatatizo, lakini si kweli hao ni matapeli,” alisema Meena katika mahojiano na Thehabari.com leo.
Hata hivyo tayari amefanikiwa kurejesha e-mail hiyo na sasa amebadili namba ya siri.
“Poleni kwa usumbufu mlioupata Ni kwaba wapo matapeli wa kimataifa waliteka ‘password’ yangu na kutuma hiyo e-mail. Mimi sijambo kabisa, nilikuwa Arusha kwenye mkutano wa wahariri na sasa nipo Dodoma.
Nimefanikiwa kurejesha e-mail yangu na kubadili ‘password’.
Poleni sana kwa usumbufu, na asanteni kwa wale walioniarifu kwa simu kuhusu tukio hili. Hivi karibuni Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) walikutaka kwenye mkutano mkuu na kujadili masuala mbalimbali ndani ya tasnia ya habari na taifa kiujumla,” ameandika leo katika mtandao wa wanabidii.
Source The habari
No comments:
Post a Comment