Thursday, July 14, 2011

MADEREVA PIKI PIKI WAENDELEA KUUAWA NA MAJAMBAZI TARIME

WIMBI la kuuawa madereva Piki piki maarufu Boda Boda wilayani Tarime Mkoani Mara la shika kasi baada ya Kijana Hamis Kitinya [16] mkazi wa eneo la Msati mjini hapa, kukutwa mwili wake katika eneo la mtaa wa Saronge mjini hapa, ukiwa umetelekezwa, baada ya kuuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Kamanda wa Polisi Tarime na Rorya Deusdedit Luta Kato alibainisha tukio hilo kuwa lilitokea usiku huo na kisha mwili wa marehemu huyo kukutwa maeneo hayo na wasamalia wema kuwajulisha Polisi kufika na kuuchukua kuuhifadhi katika chumba cha kutunzia maiti katika Hospitali ya Serikali wilayani hapa.

'' Tulipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kuwa mwendesha piki piki amekutwa eneo la mtaa wa Saronge ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye nchi kali kichwani na kisha kumpora piki piki yake ambayo ni mali ya Hellena Ndalo Kimalio'' alisema Kato.

Kwa mjibu wa kamanda huyo alisema kuwa watu hao wanaosadikika ni majambazi wasiofahamika idadi yake, baada ya kutenda mauaji hayo waliondoka na Piki piki ya marehemu huyo yenye namba za usajili T 210 BEG na kutokomea kusiko julikana.

Ilidaiwa na kamanda huyo kuwa marehemu huyo ailibainika kuwa majambazi hayo kabla ya kutenda mauaji hayo, walitumia mbinu ya kumdanganya marehemu Hamis kwa kumkodi wakidai awapeleke maeneo ambayo hayakubainika haraka licha ya marehemu yeye mwenyewe kueleweshwa majira ya usiku.


Majambazi hayo wakati wakiwa njiani wakielekea walikomhadaa marehemu huyo waliamua kutenda adhima yao na kisha kuucha mwili wa marehemu huyo maeneo ya wazi katika mtaa huo na kisha kutokomea na piki piki hiyo kusikujulikana hadi hapo mwili wa marehemu kukutwa jana asubuhi na wapita njia .

Kamanda kato alisema Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali juu ya kuwapata wale wote waliohusika na mauaji hayo na wakati tunakwenda mitamboni hakukuwa amekamatwa mtu yoyote yule aliyehusika na tuki hilo jana.

Kato aliwataka madereva Piki piki maarufu Boda Boda Mjini hapa, na wilaya za Tarima na Rorya kuwa makini na wale wanaowakodi katika muda wa usiku hata kama watawapatia fedha nyingi.


Kato ambaye amehamia hivi karibuni Tarime na Rorya baada ya Kamanda Constantine Massawe kuhamishwa aliwataka wananchi kuhakikisha wanawafichua wahalifu mara moja bila wa matukio mbali mbali waliokimbia na waliopo ili watu hao kukutana na mkono wa sheria.

Hata hivyo aliwaondoa mashaka kukosa uaminifu wa Polisi na wananchi wanaotoa taarifsa kwa njia yoyote ile kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kutunza siri za wale raia wema wanaotoa taarifa za uhalifu na Jeshi la Polisi linazingatia maadili yake na kudhibiti wale Polisi wanaokwenda kinyume.

No comments:

Post a Comment