Mwana blog leo asubuhi katika kipindi ninchokiongoza cha Big breakfast Victoria Fm ya mjini Musoma kulikuwa na mada hii hapo juu,mengi wamesema wasikilizaji lakini bado wanaonyesha viongozi ndio tatati katika hili. Walisema kuwa Tanzania sio maskini bali wananchi wa Tanzania ndio maskini,waliongeza kuwa nchi ya Tanzania ina maliasili nyingi sana ambazo ni aibu kusema kuwa nchi hii ni maskini.
Pamoja na mjadala kuwa mzuri kwa wasikilizaji wa Victoria Fm lakini ebu jiulize mtanzania kama wenye dhamana ya kututoa katika umaskini ndio hao wanaotugawanya je umaskini utaondoka? ebu Tazana kuna nchi yenye madini ya Tanzanite katika dunia hii tofauti na Tanzania? sasa iweje watu waseme Tanzania maskini?
Watanzania tuwe makini na nchi yetu maana leo kuna shule nyingi za kata ambazo zinaleta mgawanyiko na kuandaa watanzania ambao wataishi bila ajira.viwanda hakuna wasomi wanazidi kuongezeka.sasa kazi kwako mwana wa Tanzania
No comments:
Post a Comment