Wednesday, September 1, 2010

CHADEMA WAENDELEA KUNADI SERA ZAO MUSOMA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo wameendelea kunadi sera zao katika harakati za kulitwaa jimbo la Musoma mjini ambalo linashilikiwa na chama tawala chama cha Mapinduzi CCM.

Katika kujinadi huko viongozi wa CHADEMA leo jioni walikuwa katika mtaa wa Baruti kata ya Nyakato ambapo mgombea ubunge kupitia chama hicho Vicent Nyerere  alisema kama akipata kuliongoza jimbo hilo ana imani maendeleo yatakayopatikana yatakuwa tofauti na maendeleo yaliyopo sasa.

Aidha viongozi hao pia walimnadi mgombea udiwani katika kata hiyo kupitia Chama hicho Mzee Nyamwabho.

       MTANZANIA KAZI KWAKO  MIMI SIMO

No comments:

Post a Comment