TARIME
WATU wanaosadikika kuwa majambazi wamevamia baa moja katika mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Sirari wilayani Tarime na kuwaua watu wawili kwa kuwapiga risasi akiwemo askari wa jeshi la polisi.
Kamanda wa jeshi la polisi katika mkoa wa kipolisi wa Tarime na Rorya kamishina msaidizi Constantine Massawe,akiongea kwa njia ya simu na Jambo Leo alisema kuwa tukio hilo lilitokea agosti 29 mwaka huu majira ya saa 5.50 usiku katika eneo hilo
Alisema katika tukio hilo pia watu 18 wamejeruhiwa vibaya kwa kukatwa katwa na mapanga na wengine wakipigwa na vitu vizito katika sehemu mbalimbali za miili yao.
Massawe alisema kuwa baada ya majambazi hayo kuvamia baa ijulikanayo kama kwa jina la High Way bar iliyopo Sirari walianza kufyatua risasi ovyo ambapo zilimpata askari polisi D 7565 koplo Musa (45) na mhudumu wa baa hiyo aliyejulikana kwa jina la Pilly (25-30)ambao wote walifarika dunia papo hapo.
Aliongeza kuwa katika ufyatuaji huo wa risasi mbali na kumuua askari huyo lakini pia watu wengi waliokuwa katika bar hiyo walijeruhiwa huku majambazi hao wakitumia mapanga kufanya uhalifu huo
Mbali na majambizi hao kufanya mauaji hayo kamanda Massawe alisema kuwa pia majambazi hayo yalifanikiwa kupora mali malimbalimbali zikiwemo simu za mkononi za wateja ambazo hazijajulikana thamani yake.
Kamanda Massawe,alisema kuwa mpaka sasa jeshi la polisi linawashikilia watu wanane kuhusika na tukio hilo ambao walikamatwa muda mfupi baada ya tukio kutokea.
No comments:
Post a Comment